Michezo

Michezo haihitaji siasa

Wadau wa mchezo wa riadha nchini wameombwa kuja na mbinu mbadala kama kweli wana nia ya dhati ya kufufua mchezo huo kutoka ngazi ya shule za msingi, sekondari hadi vyuo vikuu kuliko kuwaachia wanasiasa wasiokuwa na ufahamu wa michezo. Wakizungumza na JAMHURI kwa nyakati tofauti, wanariadha nguli waliowahi kuiletea sifa Tanzania, wanasema miaka ya 1980-1990 Tanzania ilitisha kwenye riadha kuanzia ...

Read More »

Nani atanusuru mchezo wa masumbwi?

Wadau wa mchezo wa masumbwi nchini, wametakiwa kuingilia kati na kutafuta njia sahihi za kuunusuru mchezo huo unaoelekea kupotea kutokana na malumbano yasiyokuwa na tija kati ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na vyama vya michezo. Wakizungumza na JAMHURI kwa nyakati tofauti, wadau wa mchezo huo wameshtushwa na malumbano yanayoendelea hivi sasa baina ya baraza na vyama vinavyoongoza mchezo huo. ...

Read More »

Samatta kuitangaza Tanzania ughaibuni

Serikali sasa imeamua kumtumia Mbwana Samatta katika kuuza utalii wa Tanzania duniani. Samatta anasakata soka katika klabu ya Genk, Ubelgiji.  Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii, imetangaza nia ya kuanza kumtumia mchezaji huyo pekee anayecheza soka la kulipwa barani Ulaya.  Akizungumza na JAMHURI, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, Devota Mdachi, anasema bodi yake imejiwekea malengo ya  kuhakikisha ...

Read More »

Kuondoka Acacia aibu kwa wana Shinyanga

Kampuni ya uchimbaji madini – Acacia Gold Mine, imetoa notisi ya kutaka kujiondoa kuidhamini klabu ya Stand United ya mkoani Shinyanga, kutokana na mgogoro unaoendelea kufukuta klabuni hapo. Acacia Gold Mine, imetangaza kuvunja mkataba wa udhamini huo endapo klabu hiyo itashindwa kumaliza mgogoro huo ambao umedumu kwa muda mrefu. Mdhamini huyo ametoa notisi ya miezi mitatu. Mkataba baina ya Acacia ...

Read More »

Tumepeleka watalii Rio!

Kwa mara ya mwisho Tanzania kupata medali katika mashindano ya Olimpiki ilikuwa ni mwaka 1980 michezo hiyo ilipofanyika katika nchi ya Urusi ambapo Filbert Bayi na Suleiman Nyambui walipata medali za fedha. Katika mashindano hayo Bayi alitwaa medali hiyo kutoka katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na Nyambui aliipata baada ya kushiriki mita 5,000. Tangu kipindi hicho tumekuwa wasindikizaji ...

Read More »

Kwanini Soka la EA pasua kichwa?

Mmoja wa Makocha wenye heshima katika ukanda wa Afrika  Mashariki na Kati (EA), Adel Amrouche aliwahi kutoa  maoni yake juu ya kwa nini ukanda huu haupigi hatua katika soka. Kwa wasiomfahamu, amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Burundi na baadae kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kenya (Harambe Stars) na  vilabu kadhaa, kama DC Motema Pembe ...

Read More »

Uzalendo unatuumiza michezoni

Katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika nchini Mexico katika Mji wa Mexico City mwaka 1968 Tanzania iliwakilishwa na mwanariadha aliyefahamika kwa jina la John Stephen Akhwari kwa upande wa mbio za marathon. Kwa wale wasiomfahamu huyu ni mwanamichezo hodari wa kipindi hicho aliyekuwa na roho ya chuma na uzalendo uliotukuka kwa taifa lake. Katika mashindano hayo aliacha kumbukumbu ambayo hadi leo ...

Read More »

Serikali iwekeze katika soka

Wafuatiliaji wengi wa soka la hapa nyumbani, watakubaliana nami kuwa makocha wengi wa hapa nyumbani walioanza kufundisha soka kwenye miaka ya 1980 hadi sasa, wengi wao walipata mafunzo ya mchezo huo nje ya nchi. Hawa ni akina Sunday Kayuni, Charles Boniface Mkwasa, Abdallah Kibadeni, Salum Madadi, Rogasian Kaijage, Juma Mwambusi, Sylvester Marsh na wengineo. Ni katika miaka hiyo wakati nchi ...

Read More »

Timu za zamani zirejeshwe?

Walau sasa sura ya utaifa katika Ligi Kuu Tanzania Bara inaanza kuonekana, kutokana na kila kanda kuwakilisha timu zao kutoka kwenye mikoa husika. Katika mikoa 26 ya Tanzania Bara, ni minane tu yenye timu zinazoshiriki Ligi Kuu, mingi ikiwa na timu zaidi ya moja. Dar es Salaam ina timu tano, Mbeya ina timu mbili, Shinyanga inawakilishwa na timu mbili, Mwanza ...

Read More »

TFF mnapaswa kujitathmini

Wiki iliyopita, Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilitangaza kuufuta Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Kinondoni (KIFA) kwa kile wanachosema kuwa haukufuata utaratibu. Kamati hiyo ya TFF, iliyo chini ya Mwenyekiti Wakili Revocatus Kuul ilifikia hatua hiyo baada ya kugundua kuwa uchaguzi huo uligubikwa na madudu mengi. KIFA ilifanya uchaguzi wa marudio wiki mbili ...

Read More »

Je siasa inamaliza soka la Tanzania?

Wiki iliyopita, Serikali ilisitisha kufanyika kwa mashindano ya vijana ya Umoja wa Michezo ya Shule za Msingi (Umitashumta) na ule wa shule za sekondari (Umisseta). Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene, alitoa kauli hiyo kusitisha rasmi baada ya kuzagaa uvumi kwa siku mbili. Mwaka huu michezo hiyo ya Umisseta ilipangwa kufanyika kuanzia Juni 13 hadi Juni 22 jijini ...

Read More »

Pumzika kwa amani Keshi, Afrika yote itakukumbuka

W iki iliyopita, familia ya mpira wa miguu katika Bara la Afrika ilipata msiba mzito kwa kumpoteza nguli wa soka wa Nigeria, Stephen Keshi, ambaye ana historia ndefu nchini humo. Keshi alikuwa mchezaji katika miaka ya 1990 pamoja na Kocha wa kikosi cha ‘Super Eagles’ ambacho kilichukua Kombe la Afrika (AFCON) 2013. Ni majonzi kwa wanafamilia yote barani Afrka. Unaweza ...

Read More »

Muhammad Ali; Bondia aliyetikisa dunia

Muhammad Ali (74), bingwa wa zamani wa dunia wa ngumi za uzani wa juu na mmoja kati ya wanamasumbwi bora zaidi duniani, aliyefariki katika Hospitali ya Phoenix Area, Arizona, nchini Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita. Bondia huyo aliyetamba katika miaka ya 1960 mpaka 1980 alipoamua kujiuzuru, atakumbukwa daima kwa mchango wake mkubwa katika mchezo huo. Mwanamichezo huyo wa masumbwi, alijulikana ...

Read More »

Mafanikio ya Yanga na Tanzania kuongezwa uwakilishi CAF

Tanzania kwa sasa inabebwa na Yanga katika anga za michuano ya kimataifa, kutokana na uwezo ambao wamezidi kuuonesha kwenye eneo hilo na ligi la hapa nyumbani. Hilo halina ubishi. Hiyo imekuja baada ya Yanga kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano Kombe la Shirikisho Afrika wiki mbili zilizopita. Yanga imefuzu hatua hiyo baada ya kuitupa nje Sagrada Esperanca ya Angola ...

Read More »

Misri imebeba hatma ya Stars AFCON

Jumatano ya wiki iliyopita, Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, alitaja kikosi cha wachezaji 26 kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Kenya pamoja na ile ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) nchini Gabon, ambao watacheza dhidi ya Misri mwanzoni mwa Juni mwaka huu. Katika kikosi hicho, Mkwassa amemjumuisha nahodha ...

Read More »

Uozo kwa Aveva unamtakatisha Rage Simba

Hakuna asiyefahamu kuwa kwa sasa ndani ya Klabu ya Simba ya Dar es Salaam hali si shwari, kutokana na aina ya matokeo inayoyapata timu hiyo kwa msimu minne sasa. Simba imeshindwa kabisa kupata matokeo mazuri kutoka kwa Rais wa sasa klabu hiyo, Evans Aveva, aliyebeba mikoba ya Ismail Aden Rage. Rage aliweza kuwachanganya Yanga katika kipindi chake na kuwafanya mashabiki ...

Read More »

Madudu ya TFF na neema Yanga, Azam

Zimesalia siku chache kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ambayo ni mara ya kwanza kushirikisha timu 16. Miaka ya nyuma Ligi hiyo ilikuwa inashirikisha klabu 12 hadi 14 ambapo timu mbili za juu zilikuwa zinaenda kushiriki michuano ya kimataifa. Ila kabla ya Zanzibar haijapata uanachama Chama cha Soka cha Afrika(CAF), Tanzania ilikuwa inapata bingwa wake baada ya kucheza ...

Read More »

Pluijm: Misri ni vita

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema anakwenda Misri na timu yake vitani kuisambaratisha Al Ahly ambayo itakuwa mwenyeji wao katika mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambao inaiweka Yanga kwenye mazingira magumu kushinda ...

Read More »

Rekodi inaitafuna Yanga

Hakuna ubishi kwamba baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza, hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga imejitengenezea ugumu mchezo wa marudiano. Yanga inatarajiwa kukipiga na Al Ahly ya Misri huko Alexandrie mwishoni mwa wiki hii katika mchezo wa mkondo wa pili, na kushinda ...

Read More »

Miaka kumi tangu TX Moshi William atuache (2)

Wasifu wa TX Moshi William unaeleza kuwa majina yake halisi alikuwa akiitwa Shaaban Ally Mhoja Kishiwa. TX Moshi aliyezaliwa mwaka 1954, ameacha mke na watoto wanne – Hassan, Maika, Ramadhan na Mahada. Historia yake katika muziki inaonesha kwamba alianza tangu akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi huko Hale mkoani Tanga, ambako alikuwa akipiga muziki katika bendi ndogo zilizokuwapo mjini humo. ...

Read More »

Msuva, Ibra Ajib wanasubiri nini?

Kuna maswali mengi unayoweza ukajiuliza kwa wachezaji wa Tanzania pale wanapoona mafanikio ya Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu. Miongoni mwa maswali hayo ni kwamba wanawaza nini? Wanajifunza nini? Samatta kwa sasa anacheza soka la mafanikio katika Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, wakati Ulimwengu angali lulu katika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Kama Samatta ...

Read More »

Yanga kuvunja mwiko J’mosi?

Katika historia ya soka, timu za Tanzania Yanga ikiwamo, hazina ubavu wa kuzitoa timu za Misri kwenye mashindano. Lau Simba kidogo ambayo mwaka 2003, ilivunja rekodi kwa kuichapa Zamalek kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya wababe hao kulipa kisasi. Lakini penalti ya mwisho ya kiungo Christopher Alex Massawe, ndiyo iliyowatoa Zamalek na kuvunja mwiko wa Waarabu kuzinyanyasa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons