Kwa kutambua umuhimu wa sekta ya michezo nchini, leo @nmbtanzania imeingia makubaliano na timu ya @yangasc na kuwa Benki ya kwanza nchini kuwawezesha mashabiki na wanachama wa Yanga kupata kadi za uanachama kupitia matawi yote ya NMB yaliyoenea nchi nzima.

Baada ya kusaini makubaliano haya, ushirikiano wa NMB na Yanga utalenga maeneo yafuatayo:

 Kutumia mtandao mpana wa NMB unaojumuisha matawi zaidi ya 228 kote nchini kufanya usajili wa wanachama na mashabiki wa Yanga, wakiwemo wenye umri chini ya miaka 18. Kadi hizi maalum zitakua na nembo za Yanga na NMB.

✅Mwanachama wa Yanga atalipia Shilingi 34,000 kama kianzio cha kupata kadi ya Yanga (Shilingi 5,000 ni malipo ya kadi, 5,000 amana ya kuanzia na shilingi 24,000 ni ada ya Mwanachama kwa mwaka mzima).

✅Kadi za mashabiki ambao sio wanachama – Malipo yatakua shilingi 22,000 tu (shilingi 5,000 ni ya kadi, 5,000 amana ya kuanzia na shilingi 12,000 ni ada ya shabiki kwa mwaka mzima).

✅ Kadi hizi hazitakua za uanachama/ushabiki tu, pia zina uwezo wa kufanya kazi kama kadi ya Benki! Unaweza kufanya miamala yote ya kibenki ikiwemo kuiwekea pesa, kutoa hela katika ATM na kufanya malipo mtandaoni na katika vituo vya malipo (POS).

✅Wanachama wanaweza kupata kadi za Malipo ya Kabla (Prepaid Card) ambayo huitaji kuwa na akaunti nasi na kufanya malipo kwa kupitia mtandao au kwenye Point of Sales (POS).

✅ Wanachama na mashabiki watanufaika na huduma na ofa mbalimbali za NMB ikiwemo mikopo isiyokua na dhamana (Mshiko Fasta) na punguzo la bei wakifanya malipo kupitia NMB Lipa Mkononi (QR).

✅ Benki ya NMB itawezesha matawi ya Yanga zaidi ya 900 nchi nzima kutoa huduma za uwakala wa NMB.

✅ Mbali na huduma za uanachama, NMB itaanzisha Bima ya Mwananchi ambayo itakua na gharama nafuu.

Makubaliano haya yamesainiwa na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara NMB – Filbert Mponzi na Rais wa Klabu ya Yanga – Eng. Hersi Said na kushuhudiwa na viongozi wengine wa Benki na Klabu.

Usajili huu utaanza rasmi Julai 10, 2023 kwenye matawi yote ya NMB. Tembelea tawi la NMB lililo karibu yako kupata maelezo zaidi.

By Jamhuri