Uongozi wa Azam FC umeingia makubaliano na timu ya mpira wa miguu ya wanawake kutoka Dodoma, Baobab Queens na rasmi itakua ni timu ya wanawake ya Azam FC.

Azam wamefikia makubaliano hayo ili kutekeleza agizo la kikanuni la leseni za vilabu kutoka shirikisho la soka barani Afrika, CAF, ambapo Kwa mujibu wa kanuni mpya za CAF, klabu yoyote itakayopata nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika kuanzia msimu a wa 2023/2024, itapaswa aidha kuwa na timu ya wanawake au kushirikiana katika uendeshaji na taasisi nyingine yenye timu ya wanawake.

Azam FC itashiriki michuano ya kimataifa msimu ujao baada ya kumaliza msimu wakiwa nafasi ya nne katika ligi kuu ya Tanzania bara, ‘ NBC’ na hivyo kupata tiketi ya kushiriki michuano hiyo.

Klabu nyingine zitakazoshiriki michuano ya Kimataifa ni SIMBA SC, Yanga SC na Singida Fountain Gate FC.

By Jamhuri