Na Brown Jonas

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma ameshuhudia Timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (Tanzanite) ikiibuka na ushindi wa vikapu 69-34 vya Timu ya Taifa ya Eritrea.

Mchezo huo wa ufunguzi wa kufuzu mashindano ya mpira wa kikapu Afrika umechezwa Juni 17, 2023 katika Uwanja wa ndani wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo ya kanda ya tano yanashirikisha nchi tano ambazo ni Tanzania, Burundi, Rwanda, Sudani ya Kusini na Eritrea, ambapo timu mbili ndizo zitakazofuzu kushiriki mashindano ya Afrika yatakayofanyika mwezi Julai 2023 Nchini Angola.