Makala

Tupunguze waheshimiwa Tanzania

Neno ‘mheshimiwa’ limekosa heshima inayokusudiwa. Ni tatizo linalotokana na ukarimu mkubwa uliopo Tanzania uliosababisha kuwapo kwa idadi kubwa ya ‘waheshimiwa’ wa kila aina. Kwenye kamusi neno hilo lina maana ifuatayo: “neno la heshima linalotamkwa kabla ya kutaja jina la mtu maarufu…” Na mtu maarufu ni nani? Ni mtu anayejulikana kila mahala, au mwenye sifa za kujulikana sana. Maana isiyo rasmi ...

Read More »

Mawasiliano serikalini changamoto

Rais John Magufuli amefuta agizo la kutofungishwa ndoa kwa watu wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa kuanzia Mei mwaka huu lililotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe.  Rais Magufuli amewatoa hofu Watanzania na kuwataka kuendelea na utaratibu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na iwapo kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na ...

Read More »

Ndugu Rais umasikini wa Tanzania ni kama wa kulogwa

Ndugu Rais, yanayoandikwa katika ukurasa huu hayalengi kumpendeza mtu wala kumchukia mtu. Nchi yangu kwanza ndiyo dira; watu, vyama vya siasa na mengine baadaye! Hachukiwi mtu hapa kwa sababu imani ya ukurasa huu ni kwamba kila mtu ameumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyewe! Lengo la ukurasa huu ni moja tu! Kuililia nchi yangu, kuwalilia masikini wa nchi hii! Kukulilia na ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 37

Uvuvi ni vurugu tupu   B: Idara ya Uvuvi  697. Samaki ni moja ya maliasili muhimu kwa afya na uchumi wa taifa. Samaki wanapatikana katika mito, maziwa, mabwawa na baharini. Kwa kuzingatia umuhimu wa maliasili hii serika ilitunga sheria ya msingi ya “The Fisheries Act No. 6 of 1970,” ili kusimamia hifadhi, ulinzi na matunzo yake kwa ajili ya manufaa ...

Read More »

Mgogoro wa Israel na Palestina -12

Jibu la swali la pili linapatikana kwa mujibu wa maoni yaliyotolewa na mahakama ya kimataifa Mei 28, Mwaka 1948 kwa maombi ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Swali lililoulizwa na Balaza Kuu la Umoja wa Mataifa mbele ya mahakama lilikuwa na lengo la kupima uzito na endapo mwanachama wa UN anapoomba uananchama chini ya kifungu cha 4 cha katiba ...

Read More »

Loliondo: Wanayofichwa Rais Magufuli, Waziri Mkuu

Nayaandika haya nikisukumwa na kauli ya Rais John Magufuli, ya “msema kweli ni mpenzi wa Mungu.” Ili mambo yaweze kwenda mbele hatuna budi kuwa na ujasiri wa kuyasema mambo kwa uwazi ili kuondoa vikwazo vinavyoashiria mkwamo. Kuusema ukweli utawafanya viongozi wetu wakuu wasiendelee kulaghaiwa. Dhamira yao ni nzuri kwa hiyo kinachotakiwa ni sisi tulio pembeni kuacha woga ili tuyaseme mambo ...

Read More »

Yah: Maisha ya kufikirika bila kufanya kazi ni njozi ya mchana

Hakuna mtu asiyefikiria, hata mimi ninafikiria sana katika maisha, jambo baya zaidi ninapofikiria mimi huwa nahama mwili mzima na kuelekea kunako giza la mawazo, hii ndio sifa ya binadamu anayeweza kufikiria jambo moja kwa umakini bila kuchanganya mambo, anayeweza kufikiria jambo kwa tija na siyo kwa kuwa na ndoto za alinacha. Leo nimeondoka kidogo katika utafiti wangu ambao bado haujakamilika, ...

Read More »

Unafsi unavyoleta matatizo Tanzania

Tanzania haiwezi kuendeshwa kupata maendeleo mazuri iwapo viongozi wake ni watu wenye unafsi katika kuyaendea maendeleo ya dunia, kama kanuni za sayansi zinavyotaka na imani ya Muumba wetu inavyotaka na inavyoagiza katika kuyakabili mazingira yetu nchini. Ifahamike kwamba Tanzania ni nchi; ni jumuiya wala si taasisi kama Chama Cha Mapinduzi, Chadema au TLP.  Wala si dini ya Kiislamu, Kikristu au ...

Read More »

Wakati wa Afrika kushika hatamu unawadia

Mwenendo wa takwimu za kuzaliwa watoto duniani zinaashiria kuwa Bara la Afrika litakuwa na vijana wengi zaidi kuliko maeneo mengine ya dunia ifikapo mwaka 2050. Ni suala ambalo linatoa fursa na wajibu mkubwa kwa Bara la Afrika katika uhusiano wa kimataifa. Wastani wa ongezeko la watu barani Afrika ni asilimia 2.5; ikilinganishwa na wastani wa dunia wa asilimia 1.2. Ipo ...

Read More »

Madhara ya kuacha ujamaa Tanzania

“K una namna tatu za kuendeleza usawa (Ujamaa) zaidi nchini mwetu. Kwanza ni kupunguza tofauti ya kipato baina ya watu. Ya pili ni jinsi huduma (afya, elimu nk) za jumuiya zinavyomfikia kila mtu, na kiasi ambacho huduma hizo ambazo hugharamiwa kwa kodi za wote, zinawafaa watu wote, na siyo kikundi cha watu wachache tu. Na ya tatu ni wananchi kushirikishwa ...

Read More »

Ni hatari kuua biashara

Leo nimeona niandike mada inayogusa maisha ya kila Mtanzania –  biashara. Naandika mada hii kutokana na mwenendo usioridhisha unaoonesha kuwa biashara nyingi hapa nchini zinakufa.  Kwa muda mrefu tumekuwa tukiambiwa kuwa Tanzania ni taifa la wakulima na wafanyakazi. Ni kwa bahati mbaya, hao wakulima na wafanyakazi wanastahili heshima, ila uchumi una misingi yake. Kwa siku za karibuni wafanyabiashara wengi hapa ...

Read More »

Makala: Tunamaliza mgogoro Mbarali

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala, amesikiliza kilio cha wananchi na kuanzisha mchakato kufuta Tangazo la Serikali Na. 28 la mwaka 2007 lililoweka mpaka mpya kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo chini ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wananchi wakazi wa Wilaya ya Mbarali. Februari 27, mwaka huu ilikuwa siku ya pekee kwa wakazi wa ...

Read More »

Mtaji sekta ya kilimo kikwazo cha uchumi

Serikali imetakiwa kuangalia kwa mapana sekta ya kilimo pamoja na kukubali kufanyia kazi kwa vitendo ushauri unaotolewa na wataalamu wa kilimo na uchumi kwa ajili ya kufanya maboresho katika sekta hiyo. Kutokana umuhimu wa kilimo katika kufanikisha Tanzania ya Viwanda. Mtaalamu wa Uchumi wa Kilimo, Profesa Anna Tibaijuka, amesema kuwa kinachokwamisha maendeleo katika sekta ya kilimo hapa nchini ni ukosefu ...

Read More »

Haya matukio yanaashiria nini? (2)

…Hivyo hatua ya kwanza kutekeleza mfumo mpya wa utawala kutoka ule wa ukoloni tuliorithi mwaka 1961, na ambao umetumika mpaka wakati ule mwaka 1971, ilikuwa kuteua viongozi wakuu wa kisiasa kwa mikoa na wilaya.    Hawa waliitwa Wakuu wa Mikoa (Regional Commissioners-RCs) ambapo enzi za ukoloni wakiitwa Provincial Commissioners-PCs, Wakuu wa Wilaya ndiyo hao wakiitwa District Commissioners-DCs, sasa sisi tukaja ...

Read More »

Yah: Utafiti wangu katika mambo madogo madogo ya uswahili

Kuna watu wanaona kama maisha yamekuwa magumu kupitiliza, mimi nawaunga mkono kwamba maisha ya sasa ni shughuli pevu kwelikweli kutokana na ukweli wa mabadiliko ya sera. Tulianza kwa kushangilia hotuba mbalimbali za viongozi na matamko ambayo baadhi yetu hatukuelewa kwamba tunarudi Tanzania ambayo ilikuwa imepotea. Leo hii kila kaya, kila kona na kila mtu wimbo ni mmoja tu kwamba maisha ...

Read More »

Nyakati tatu za dua kujibiwa (2)

Wiki iliyopita, katika sehemu ya kwanza ya makala hii, nilielezea kilio cha muda mrefu cha Watanzania kuhusu hali ya jamii kimaisha siyo nzuri na sheria za nchi hazifuatwi, kama ilivyoandikwa na gazeti moja nchini, mwaka 2013. Nilinukuu aya ya kwanza na ya 42 ambazo zilionesha ni kilio, dua na maombi kwa Mwenyezi Mungu kutoka kwa Watanzania wakihitaji mabadiliko ya uongozi ...

Read More »

Kupata hati unaponunua ardhi ya kijiji kwa uwekezaji

K awaida hatimiliki (granted right of occupancy) hazitolewi kwa ardhi za vijijini. Ardhi za mijini ndizo zilizo na hadhi ya kupata hatimiliki. Lakini wapo watu ambao wamechukua maeneo ya vijijni kwa ajili ya uwekezaji.   Wapo waliochukua ardhi kama wachimbaji wadogo, kilimo, madini, n.k. Hawa pengine wangependa wapate hatimiliki ili kukuza biashara zao sambamba na kupata faida zinazotokana na kuwa ...

Read More »

Nahisi demokrasia yetu inahitaji fasili mpya (1)

Demokrasia inatafsiriwa kuwa: mfumo wa kuendesha serikali iliyochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu. Tafsiri haina tatizo, lakini yapo mambo yanavyoweza kutokea ndani ya mfumo huo ambayo yanaweza kusababisha hitilafu kubwa. Kwa utaratibu wetu, kila baada ya miaka mitano vyama vya siasa “vinajinadi” kwa wapiga kura halafu ndani ya siku za mwishoni mwa mwezi wa Oktoba wa mwaka wa uchaguzi, ...

Read More »

Ng’ombe 1,000 wanaliwa Dar kila siku

Ng’ombe 1,000 wanaliwa kila siku jiji Dar es Salaam. Takwimu hizo zimepatikana katika machinjio yote yaliyoko jijini.  Hali hiyo imesababisha ongezeko la mapato kutoka Sh milioni 4 hadi Sh milioni 8 kwa siku katika Mnada wa Mifugo Pugu, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli, uchunguzi ...

Read More »

Mgogoro wa Israel na Palestina – 9

Madhumuni ya Mamlaka:  Dhana ya Mamlaka za Kimataifa (International Mandates) zilichagizwa na Rais Wilson na viongozi wengine wa mapinduzi ya Russia na ukomo wa vita katika Vita ya Kwanza ya Dunia isingehusisha mmego wowote (annexation), lakini ingekatika katika Kanuni Kuu ya Uhuru wa kujiamulia mambo ya watu. Pendekezo mahususi la dhana ile lilitolewa na General Smuts kama sehemu ya mradi ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 35

Wagawa viwanja barabarani Ugawaji wa nyumba za Shirika la Nyumba (NCH)   663. Kwa muda mrefu kumekuwepo na malalamiko miongoni mwa wananchi kuhusu ukiukwaji wa utaratibu unaotumika katika kugawa nyumba za Shirika. Baadhi ya waombaji wa nyumba hizo wamejaza fomu za maombi miaka mingi iliyopia na kila wakifuatilia maombi hayo wanajibiwa kwama hakuna nyumba zilizo tupu. Hata hivyo, kuna baadhi ...

Read More »

Usalama wa wachimbaji wadogo, changamoto kubwa

Mkoa wa Geita, ambao umetawaliwa na shughuli za uchimbaji madini, sasa unakabiliwa na changamoto za usalama kazini katika machimbo yanayowahusisha wachimbaji wadogo. Moja ya matukio hayo ni pamoja na lile lililotokea usiku wa kuamkia Januari 26, mwaka huu ambapo watu 15 – mmoja akiwa raia wa China – walinusurika kufa kwa kufukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ Union, unaomilikiwa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons