CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI

Diwani wa Kata ya Haneti Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Peter Elia Chidawali akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo ‘Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima’ Wilayani Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja akitambulisha Kampeni ya Kitaifa ya Kuzuia Mimba za Utotoni kwa wanafunzi wa shule sambamba na utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatil idhidi ya Wanawake na watoto katika Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Shukuru Shanjala akiwaasa watoto wa kike kujitambua na kujilinda dhidi ya mimba za utotoni ili kupata haki ya kuendelezwa na kutoa mchango katika kufikia uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia mimba za utotoni Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakisikiliza ushauri wa malezi na makuzi kutoka kwa wataalamu jinsia ili kuwawezesha kupambana na mimba za utotoni wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Afisa Maendeleo Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya msingi na sekondari Haneti Wilayani Chamwino kuhusu kupambana na Mimba za utotoni katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Afisa Maendeleo Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akitoa vipeperushi kwa wanafunzi wa Shule ya msingi na sekondari Haneti Wilayani Chamwino kuhusu kupambana na Mimba za utotoni katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakisoma vipeperushi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakionesha vipeperushi mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Diwani wa Kata ya Haneti Mhe. Peter Elia Chidawali(wanne kulia) akiwa katika picha na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Rose Minja(wa tatu kulia) pamoja na waalimu na wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari Haneti mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani Chamwino.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
 
Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma imejipanga kupambana na kutokomeza mimba za utotoni katika Wilaya hiyo.
Akizungumza katika uzinduzi wa Kapeni ya Kutokomeza Mimba za Utotoni katika Shule za Msingi na Sekondari katika Kata ya Haneti Wilayani Chamwino Diwani wa Kata ya Haneti Mhe. Peter Elia Chidawali amesema kuwa Kata yake na Wilaya kwa ujumla wamejipanga katika kupambana na vitendo vya ukatilia wa kijinsia yakiwemo matukio ya mimba na ndoa za utotoni .
Mhe. Peter Elia Chidawali ameongeza kuwa hawatakubali kuona watoto wao wanapoteza haki yao ya msingi ya kuendelezwa ya kupata Elimu kwa kupata mimba au kuolewa wakiwa bado shuleni.
“Tutaendeleza Kampeni katika ngazi za familia kwa kuwaelimisha wazazi na walezi kuhusu madhara ya mimba za utotoni ili tuokoe kizazi cha kesho”alisema Mhe. Chidawali.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja amesema kuwa suala la mimba za utotoni limezidi kuongeza siku hadi siku hivyo basi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alizindua Kampeni ya Kutokomeza Mimba za utotoni kwa lengo la kuwezesha utoaji wa  elimu kwa wanafunzi, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kushiriki mapambano dhidi tatizo hili.
“Wanafunzi, Walimu, Wazazi na walezi tuweke mikakati thabiti ya kupambana na tatizo hili la mimba za utotoni” alisisitiza Bi. Rose.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Shukuru Shanjala ameeleza kuwa Wilaya ya Chamwino imejipanga katika kuzuia mimba za utotoni kwa kuhakikisha wanawafikia wahusika katika ngazi za shule na familia na kutoa elimu kwa watoto wote wa kike wanaowazunguka ili kuondokanana tatizo la mimba za utotoni katika wilaya yao.
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea na kampeni ya kuzuia mimba za utotoni chini katika shule za Msingi na Sekondari ijulikanayo kama Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima sambamaba utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na watoto katika ngazi mbalimbali nchini ili kupunguza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/2022.
1019 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!

Comments

comments

Show Buttons
Hide Buttons