Messi: Inaniuma sana kukosa penalti Kombe la Dunia

Lionel Messi amesema inamuumiza sana baada ya Penati yake dhidi ya Iceland kuokolewa wakati Argentina ilipokutana na Iceland.

Mkwaju wa penati wa Mchezaji huyu,30 na nyota wa Barcelona haukuleta madhara mbele ya mlinda mlango Hannes Halldorsson na kufanya timu hizi mbili kutoka sare ya 1-1

Messi alikuwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema akitazama matokeo ya hasimu wake wa siku nyingi Cristiano Ronaldo hasa mabao matatu aliyoyafunga siku ya ijumaa dhidi ya Uhispania.

”Tumepata uchungu kwa kukosa alama tatu, kuanza kwa ushindi ni muhimu sana wakati wote, sasa tunapaswa kufikiria kuhusu Croatia”.

”tutajitahidi kuhakikisha hili linapita haraka”.

Messi alisema mbinu ya Iceland ilifanya mchezo ukawa mgumu ”hawakutaka kucheza” lakini alikiri kuwa walijihami kwa ”kiasi kikubwa”

 

700 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!

Comments

comments

Show Buttons
Hide Buttons