Muslim Hassanali, aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ilala 2015.

ALIYEKUWA mgombea ubunge Jimbo la Ilala kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa 2015, Muslim Hassanali, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi  (CCM)  na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na viongozi wengine wa CCM katika ukumbi wa Checkpoint Pugu jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula (katikati)akiwa na viongozi wengine.

Kujiunga kwa Hassanali ni mwendelezo wa mfululizo wa viongozi wa upinzani wakiwemo wabunge na madiwani kuondoka na kwenda CCM.

Muslim Hassanali (kushoto) akirudisha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Ilala kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi mkuu wa  2015.

Viongozi kadhaa wakiwemo wabunge na wapinzani wamejiunga na CCM wakitokea upinzani kwa sababu mbalimbali  ikiwemo ya kuunga mkono serikali ya Rais John Magufuli.

1182 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!