Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametembelea ujenzi wa ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar.


Ujenzi huo unahusisha jengo la utawala, ukumbi pamoja vitega uchumi mbalimbali kama vile maduka.

Mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa Jengo hilo, Makamu wa Rais amewasihi wanachama wa CCM kuendelea kujitoa kwaajili ya chama hicho.

Amesema tangu wakati wa vyama vya TANU na ASP ambavyo viliunda CCM vyama hivyo vilijengwa kwa nguvu za wanachama.

Amewapongeza wanachama wa CCM Wilaya ya Micheweni kwa hatua nzuri iliyofikiwa na mawazo waliyonayo juu ya jengo hilo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi ya Wilaya hiyo tarehe 21 Aprili 2024.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM – Zanzibar Khamis Mbeto Khamis (kushoto) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar wakati alipotembelea na kukagua jengo hilo tarehe 21 Aprili 2024.
Please follow and like us:
Pin Share