Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 17, 2018 amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za Serikali za msingi na Sekondari na kuwaagiza Mawaziri Jafo na Ndalichako kusimamia hilo.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo mara baada ya kufanya kikao na waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo na waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako Ikulu Jijini Dar es salaam na kuagiza ufuatiliaji wa karibu wa agizo hilo.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa kama kutakuwepo na mchango wowote wa mzazi ambaye atajisikia kuchangia jambo lolote kuhusu masuala ya shule basi pesa hizo zipelekwe kwa Mkurugenzi na si kushikwa na mwalimu yoyote yule

Kumekuwa na mtindo wa kuwarudisha nyumbani baadhi ya wanafunzi katika shule za umma kutokana na kushindwa kutoa michango ambayo ipo nje ya utaratibu wa ada hali iliyomkera Rais Magufuli na kuingilia kati hali hiyo.

By Jamhuri