Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Pwani

Mkuu wa mkoa wa Pwani alhaj, Abubakar Kunenge amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Mazingira ya Kituo cha Mabasi kibaha (Kibaha Bus Terminal), ambapo amepokea kero ya kuchelewa kufika kwa  Mabasi ya Mwendekas  kituoni hapo ambayo yanafanya safari zake Kati Kibaha  -DSM.

Akiwa kwenye ukaguzi huo,  Kunenge amesikiliza kero za wananchi waliokuwemo eneo hilo. 

Vilevile wananchi hao wameeleza kutotosheleza kwa vikingia jua na Mvua zilizojengwa kwenye Eneo hilo na Kujaa kwa maji kwa baadhi ya maeneo yanayotumiwa na Mabasi  ya mwendokasi na Mabasi madogo kwenye eneo hilo.

Akijibu kero za Wananchi Kunenge ameeleza Nia ya Rais na wasaidizi wake ni kutatua kero za Wananchi na kuwarahisishia utoaji wa Huduma.

Kunenge ameeleza kero zote amezichukua na zinakwenda kufanyiwa kazi. 

Kuhusiana na Mabasi ya Mwendokasi amewasiliana na mamlaka husika kwamba huduma hiyo kwa sasa hairidhishi na hivyo  wameahidi kuongeza mabasi hayo na viongozi wa DART kutembelea eneo hilo. 

Kuhusu kuharibika kujaa maji na mabonde kwenye kituo hicho ameagiza wataalam wa Halmashauri kushirikiana na TANROADS na TARURA kufanya matengenezo ya maeneo yaliyoharibika.

By Jamhuri