Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omar Kumbilamoto amewaasa wafanyabiashara kufanya biashara kwa kutumia mitandao ikiwa na lengo kukuza biashara zao.

Ameyasema hayo leo Mei 2, 2024, alipoakizindua duka la simu la Maandasi Store lililopo Banana jijini Dar es Salaam.

Kumbillamoto amesema kuwa dunia ya sasa inahitaji mfanyabiashara kutumia mawasiliano ikiwa kama sehemu kuwafikia wateja kwa urahisi ambapo kwa kufanya hivyo kutaweza kutangaza biashara husika na hatimaye kukuza na mitaji yao na hatimaye kulipa kodi kwa nchini ambayo inaleta maendeleo kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi Mtendaji duka hilo, Abdilah Omar Juma amesema kwa sasa wao wanalenga kuwawezesha Wananchi wote kumiliki simu kwa gharama nafuu ikiwa pamoja na kuwakopesha kwa utaratibu wa kulipa kidogo kidogo kwa muda watakao kubaliana.

Aidha pia mteja atapewa utaratibu na hatimaye kulipa kwa urahisi bila usumbufu wowote, mstahiki Meya hivyo amewaomba Wananchi wote kwenda kwenye duka hilo na kujipatia simu bora na za kijanja.

Kampuni ya maandasi ina miliki maduka yapatayo 14, katika mikoa 10, Tanzania nzima huko makao makuu yakiwa ni hapo Banana, Jijini Dar es Salama.

Katika hatua nyingine Meya huyo,amekemea tabia ya baadhi ya watu kutumia mitandao kinyume na utaratibu hivyo Jambo linalopekea mmong’onyoko WA maadili kwa vijana wengi na watoto.

By Jamhuri