Na Isri Mohamed

Beki wa Coastal Union Lameck Lawi amefutiwa adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa na mwamuzi wa mchezo dhidi ya Yanga Sc baada ya kuthibitika kuwa mwamuzi huyo wa kati pamoja na mwamuzi msaidizi namba mbili kushindwa kutafsiri vyema Sheria za Mpira wa Miguu katika tukio la mchezaji huyo kumvuta jezi kiungo wa Yanga Stephanie Ki Aziz.

Kamati ya TFF ilipokea taarifa za uchambuzi wa kitaalam kutoka kwa wakufunzi wa waamuzi, ambazo zimeainisha kuwa mchezaji huyo hakustahili kuonywa kwa kadi nyekundu badala yake ilipaswa aonywe kwa kadi ya manjano kwasababu wakati tukio linatokea, kulikuwa na mlinzi mwingine wa Coastal Union mbele yake ambaye angeweza kuufikia mpira.

Mwamuzi wa kati na mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo huo wamepewa Onyo Kali kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu katika tukio hilo liliishuhudia Coastal Union wakimaliza mchezo wakiwa pungufu na kupoteza 1-0 dhidi ya Yanga Sc.

By Jamhuri