Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma

Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao ( e-GA) imejipanga kutumia mifumo ya teknolojia kurahishisha utendaji kazi wa watumishi wa umma.

Hayo yameelezwa leo Aprili 28,2023 Jijini Dodoma na Afisa TEHAMA kutoka Utumishi Bw.Hossea Laizek,akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la e-GA wakati wa kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizika leo Aprili 28,2023 kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Amesema kupitia mfumo wa E mrejesho watumishi wanaweza kufuatilia taarifa mbalimbali kuhusu malalamiko,pongezi na huduma mbalimbali zinazotolewa katika ofisi.

Pia amesema kuna mfumo wa watumishi porto ambao unaweza kuwahudumia watumishi wa uuma bila ya kufika katika kituo cha kazi ikiwa ni pamoja na kufanya uhamisho.

“Kuna huduma nyingine inawezesha watumishi kupanga plan zao za mwaka na kurekodi utendaji kazi wake wa kazi,”amesema Laizek

Kwa upande wake Afisa TEHAMA kutoka Mamkala Mtandao (e-GA) Tumaini Masinsi amesema kupitia maonesho hayo kuna mfumo uitwao Oxgen Net ambao ni wa Whatsup ya ndani.

“Oxgen ni chatting platform ni ya hapa ndani kwa ajili ya kuchat na kwa ajili ya video Call na kwa ajili ya kujifunza vitu mbalimbali.Namna ya kuipata unaweza kutumia Web Oxgen Net na kuitumia na katika Playstore,”amesema

Amesema katika maonesho hayo wamekuja na bunifu mbalimbali za mfumo kwenye mambo ya tehama ambazo zimefanywa na vijana wabunifu wazalengo.

“Tuna bunifu mbalimbali ambazo zimefanya na wabunifu wazalendo kwa ajili ya kurahisisha vikao vya madaniwani na Halmashauri ikiwa ni pamoja na kuweka vizuri agenda,”amesema

Pia amesema wana E dodoso imetengezwa kwa ajili ya watafiti kukusanya data na kuchakata ambazo zitarahishisha uandishi wa ripoti mbalimbali.

Naye,Afisa TEHAMA kutoka Mamlaka Mtandao Vannesa Mhando amesema wao kama vijana wanajifunza uzalendo na kutiwa moyo kuendelea kutengeneza suluhu ambazo zitatua matatizo ya watanzania.

Amesema wanajiendeleza kiteknolojia kwa ajili ya kukuza ujuzi na kuendeleza mambo mazuri.

By Jamhuri