Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud wakati alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa katika mapokezi kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud wakati alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.
Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud akisaini kitabu cha wageni mbele ya mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya Kiserikali tarehe 27 Aprili 2024.
Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud akikagua gwaride wakati wa mapokezi rasmi katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo ya pamoja na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud na Ujumbe wake yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili, 2024.

By Jamhuri