Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Morogoro

Waziri wa habari, Mawasiliono na Teknolojia ya habari Nape Nnauye amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuimarisha sekta ya habari ikiwa ni pamoja na kuzipitia sheria zinazolalamikiwa na wadau ikiwemo sheria ya huduma za habari namba 12 ya mwaka 2016.

Hayo ameyasema wakati akifungua mkutano wa 12 wa kitaaluma wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF),mkoani Morogoro uliohudhuriwa na wahariri 130 ambapo ukiongozwa na kauli mbiu ya ‘Sheria ya Habari na Maendeleo ya Vyombo vya habari’.

Nape amesema amesema kuwa nia njema ya Serikali ni kuwa na sheria nzuri za habari zitakazodumu kwa muda mrefu zaidi na sio sheria kandamizi zinazotiliwa shaka na wadau wa habari.

“Kati ya mambo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuimarisha sekta ya habari kwa kuzipitia sheria zinazolalamikiwa na wadau ikiwemo sheria ya huduma za habari namba 12 ya mwaka 2016,” amesema.

“Hata hivyo ninawahakikishia wahariri kuwa marekebisho ya sheria ya Huduma ya habari ya mwaka 2016 tayari yapo bungeni, nawasihi muwe na subira” amesema.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inatambua na kuheshimu mchango wa sekta ya habari katika kuimarisha uchumi na utawala bora hivyo ni vyema kuwa na sheria zenye kuleta usawa na haki ya upatikanaji wa habari.

Waziri Nape ameongeza kuwa hata hivyo kumekuwa na mabadiliko makubwa katika utendaji wa vyombo vya habari hivyo akalitaka Jukwaa la Wahariri wa Habari kuendelea kuwapa mafunzo waandishi wa mitandaoni kwa lengo la kuripoti habari zilizochakatwa kisahihi.

‘Baadhi ya waandishi wa mitandao ya kijamii nchini wamekuwa wakiripoti habari ambazo hazina mizania sababu mojawapo ikiwa ni pamoja na kukosa ueledi wa taaluma ya habari na kuleta mitafaaruku kwa jamii na serikali,” amesema.

“Muwaelekeze waandishi wa habari za mitandaoni ambao wengi wao wamekuwa wakipotosha maadili ya uandishi wa habari jambo ambalo litasaidia kupunguza kesi dhidi ya vombo vya habari na serikali..Tukifanya vizuri jamii itatuheshimu na tukifanya vibaya jamiii itashangaa ”amesema waziri Nape.

“Nidhahili kuwa Jukwaa la wahariri linamchango mkubwa kwa sarikali katika kuhakikisha habari zinazopatikana zinakuwa hazileti mtafaaruki kwa jami hivyo serikali inatambua mchango wenu,” amesema.

Waziri Nape pamoja na mambo mengine amewataka waandishi wa habari kuendelea kuandika habari za uchunguzi ili kuibua changamoto zilizopo kwenye jamiii kusaidia serikali kutekeleza majukumu yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF), Deodautus Balile amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwa imekuwa tangu iingie madarakani kumekuwa na mabadiliko makubwa katika ushirikiano na vyombo vya habari.

“Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwani imekuwa na ushirikiano mzuri na vyombo vya habari licha ya kuwepo kwa baadhi ya vipengele ambavyo vimekuwa kikwazo na kulalamikiwa na wadau wa habari na kuhitaji kufanyiwa marekebisho.

“Hata hivyo kumekuwa na ushirikiano mkubwa kati ya Jukwaa la wahariri, wadau wa habari pamoja na waandishi wa habari jambo lililochangia kupungua kwa kesi nyingi mahakamani zinazohusisha vyombo vya habari hapa nchini.

“Katika kipindi kifupi kuna kesi nyingi za vyombo vya habari zinazofikishwa mahakamani zimepungua, hii ni kutokana na jukwaa hili kuwa karibu zaidi na vyombo vya habari katika kuelekeza namna ya kufuata maadili ya uandishi wa habari” amesema Balile.

By Jamhuri