Mawaziri Walioteuliwa na Rais Magufuli Kuapishwa Leo

Mabadiliko, haya yalifanyika ambapo,

RAIS John Magufuli jana amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kwa mujibu wa taarifa yake iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng .John Kijazi mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:

Kangi Lugola, aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) sasa anakuwa  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo amechukua nafasi ya Mwigulu Nchemba.

 

Musa Ramadhani Sima amekuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

 

Omary Mgumba anakuwa  Naibu Waziri wa Kilimo.

 

Prof. Makame Mbarawa aliyekuwa Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anakuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

 

Mhandisi Isack Kamwelwe anakuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

 

Athumani Kihami ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

 

1743 Total Views 3 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!

Comments

comments

Show Buttons
Hide Buttons