Ujumbe huu umeandikwa leo na Waziri January Makamba katika ukurasa wake wa Twitter ikiwa ni ushauri kwa wasanii na vijana maarufu. Ushauri huu umechukuliwa na wengi wa watumiaji wa mitandao ya Twitter na Instagram kama muhimu kwa wasanii hasa baada ya kuibuka kwa matendo yasiyoakisi taswira njema kwa jamii kwa siku za karibuni. Ujumbe huo umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza lakini tafsiri isiyo rasmi ni:

“Kwa wadogo zangu maarufu wa kike na wa kiume: umaarufu unabeba majukumu. Ushike kwa makini. Umaarufu unaweza kudumu kwa dakika 15 watu tukafurahi na kukuona muhimu – kisha maisha yakaendelea. Umaarufu pia unaweza kudumu milele, ukafa kimwili lakini jina lako lisife. Umaarufu pia unaweza kudumu na kufikia kiwango cha kukuharibu na kukuondoa kwenye mstari.”

Mmojawapo ya wasanii waliojibu ujumbe huo Twitter ni Vanessa Mdee ambaye ameshukuru na kusema kuwa umaarufu kweli ubabe majukumu.

Convo hii hapa chini. Unaweza ku-click picha kwenda Twitter.

 

918 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!