Watoto mapacha Nyakato (mvulana) na Nyangoma (msichana) wakazi wa Kijiji cha Butahyaibeba wilayani Bukoba wenye umri kati ya miaka minne na mitano wameuawa kwa kuchinjwa na mtu aliyedaiwa kuwa ni baba yao mzazi usiku wa kuamkia jana.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bulambizi, dickson Barongo ambako mauaji hayo yametokea, alieleza kuwa watoto hao walichinjwa na kutenganishwa vichwa na viwiliwili.

“Nilikuwa wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio baada ya kufuatwa nyumbani na mtoto aliyenusurika,” alisema Barongo.

Barongo alisema kuwa mama wa watoto hao alikimbia wakati mumewe akifanya tukio hilo ili kujinusuru.

Imeelezwa kuwa, kabla ya kufanya mauaji hayo, mzazi huyo aliwachukua watoto hao na kuwafungia chumbani.

“Chanzo cha mauaji hayo kinahusishwa na ugomvi kati ya wanandoa hao,” alisema.

Inadaiwa kuwa baada ya wanandoa hao kutengana, mwanamke alienda kuishi kwao akiwaacha watoto na baba yao.

“lakini juzi alipofika hapo kwa mume wake, akawaomba wakamtembelee Alhamisi ya wiki iliyopita na juzi (Jumamosi) alikuwa amewarudisha kwa baba yao,” alisema.

“Mume alimruhusu mzazi mwenzake kuondoka na watoto hao na siku ya tukio alikuwa amewarejesha kwa baba yao, lakini baba alimzuia ,ke wake kuondoka na akafunga mlango, lakini wakati wa vurugu hizo alifanikiwa kutoroka,” alisema.

Barongo aliongeza kuwa walimpata mtuhumiwa kwa njia ya simu na akawajibu kuwa bado hajamaliza kazi na baadae simu yake haikupatikana.

Msimamizi wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, Gloria mpango alisema uchunguzi wa awali unaonyesha watoto hao walichinjwa na kutenganishwa vichwa na viwiliwili na wanasubiri taratibu za polisi kabla ndugu kuruhusiwa kuchuukua miili kwa mazishi.

Chanzo: Mwananchi

By Jamhuri