Na Mwandishi Wetu, JAMHURI MEDIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amempokea na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Davi Harris mbele ya waaandishi wa habari leo Machi 30, 2023 Ikulu ya Dar es Salaam

Viongozi hao wawili wamezungumzia masuala mbalimbali yanayozuhusu nchi zote mbili na Dunika kiujumla Katika nyanja za kidiplomasia, ulinzi na usalama, afya pia katika masula ya ushirikiano kibiashara bana ya Tanzania na Marekani.

Viongozi hao wamegusia suala la demokrasi katika nchi ya Tanzania kwamba imeimarika kwa kiasi chake, naye Makamu wa rais wa Marekani ameipongeza Tanzania katika kuhakikisha inasimamia vizuri masuala ya demokrasia kwa kuruhusu mikutano ya vyama siasa nchini humo.

Akizungumzia Suala la afya Rais wa Tanzania amesema maambukizi ya Ukimwi kifua kikuu na maralia yamepungua kwa kiasi kikubwa hivyo yamekuwa siyo tisho tena katika taifa hilo.

Pia Rais Samia ameishukuru Marekani kwa kuirejesha Tanzania kwenye mpango wa “Feed the Future” ambao huangazia suala la usalama wa chakula pia ameitaka Marekani kufanya mapitio na kurekebisha mkataba wa Visa utakaowawezesha watanzania waishio Marekani kuwa na Visa ya mda mrefu.

Kamala Harris anatarajiwa kuhitimisha ziara yake ya siku tatu nchini Tanzania hapo kesho na kuelekea nchini Zambia ili kukamilisha ziara yake barani Afrika katika nchi tatu

By Jamhuri