Na Tatu Saad,JAMHURI MEDIA

Watu 10 wajeruhiwa na Fisi katika kijiji cha Nyamalimbe kata ya Nyamalimbe wilayani Geita mkoani Geita.

Fisi huyo aliwajeruhi raia 10 muda mfupi baada ya kumuua ng’ombe mmoja kati ya ng’ombe waliokuwa wakichungwa na watoto ambao walipiga kelele za msaada kwa wananchi baada ya kumuona fisi huyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Bethaneema Mlayi amesema Fisi huyo ameuliwa na mamlaka ya uhifadhi wanyamapori na misitu, Geita (TFS) mara baada ya kupewa taarifa na jeshi la polisi na kuwasili haraka eneo la tukio.

Mlayi amesema majeruhi wote wanaendelea vizuri na wanapata huduma katika hospitali ya Teule ya Rufaa mkoa wa Geita na wanaweza kuruhusiwa kurudi nyumabni ifikapo jioni kama afya zao Zitakuwa timamu.

By Jamhuri