Habari za Kimataifa

RAIS WA ZAMANI WA LIBERIA ELLEN JOHNSON SIRLEAF ASHINDA TUZO YA KIONGOZI BORA WA AFRIKA INAYOTOLEWA NA MO IBRAHIM

Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ameshinda tuzo ya mwaka ya Mo Ibrahim kwa Uongozi wa Afrika – ambayo hupewa viongozi wa Afrika ambao wameonekana kuwa na utawala mzuri. Ellen Johnson Sirleaf amekuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya Urais mwaka 2006 na kumaliza muda wake mwezi uliopita baada ya kuhudumu kwa mihula miwili. Kamati ya ...

Read More »

ANGALIA MADHARA YA KUJIPIGA PICHA MWENYEWE (SELFIE) UKIWA KWENYE MAENEO YA HATARI

Mwanamke mmoja amefariki akipiga picha aina ya Selfie na rafikiye katika barabara ya treni nchini Thailand. Rafikiye alisema kuwa walikuwa wamekunywa pombe na kuamua kujipiga picha hiyo na treni lakini hawakuona treni nyengine iliokuwa ikija kutoka barabara nyengine ya treni, kwa mujibu wa polisi. Miguu yake ilikatika na kufariki hospitalini ambako alikuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi. Rafikiye wa kiume alipata ...

Read More »

HATMA YA RAIS JACOB ZUMA KUNG’ATUKA MADARAKANI KUJULIKANA LEO

  Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma. Akizungumza kaika mkutano wa hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu. Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa ...

Read More »

Magaidi Wawili Hatari wa IS Wakamatwa

  Taarifa zinasema kuwa raia wawili wa Uingereza wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislam cha IS wanashikiliwa na kundi la wapigaji wa Kikurd. Alexanda Kotey mwenye umri wa miaka 34 na mwenzake El Shafee Elsheikh mwenye miaka 29 ni miongoni mwa vijana wawili waliokuwa wanasakwa kati ya wenzao ambao walikwisha kukamatwa. Kundi hili la vijana wanne kutoka ...

Read More »

WATU ZAIDI YA 20 WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LA ANGA NCHINI SYRIA

Takriban watu 23 wameuawa hadi sasa katika mashambulio ya anga ya vikosi vya serikali nchini  Syria katika eneo la mashariki mwa Ghota karibu na mji wa Damascus, kuna kodaiwa kuwa ni ngome ya waasi. Waangalizi wa haki za binadamu kutoka Uingereza waliopo katika maeneo hayo wameelezea hali hiyo na madhara kwa watu kutokana na mashambulio hayo. Umoja wa mataifa umetoa ...

Read More »

KOREA KASKAZINI KUONYESHA UIMARA WA JESHI LAKE KABLA YA OLIMPIKI

Korea Kaskazini linatarajiwa kuandaa maadhimisho ya 70 ya gwaride la jeshi lake kabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini. Gwaride la kila mwaka la Pyongyang linaloadhimisha kuanzishwa kwa jeshi la Korea Kaskazini limekuwa likifanywa kila mwezi Aprili kwa kipindi cha miaka 40. Hatahivyo vyombo vya habari nchini humo vilitangaza mapema mwaka huu kwamba ...

Read More »

MKUTANO WA KUMNG’OA ZUMA MADARAKANI WAAHIRISHWA

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeahirisha mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho ulio tarajiwa kujadili hatima ya rais Zuma. Hata hivyo badala yake taarifa iliyotolewa na chama hicho imeeleza kuwa wamekuwa na mazungumzo yenye ufanisi mkubwa na rais Zuma. Rais Zuma yupo katika wakati mgumu kufuatia shinikizo la kumtaka aachie madaraka ambalo linatoka ndani ya chama chake,halikadhalika ...

Read More »

Dada wa Mowzey Radio Akamatwa na Polisi Uganda

  Polisi nchini Uganda wamemkamata mtuhumiwa anayehusishwa na mauaji ya mwanamuziki maarufu Mowzey Radio, aliyefariki kutokana majeraha aliyoyapata baada ya mzozo uliotokea kwenye kilabu moja ya usiku ” De Bar”, iliyopo katika mji wa Entebbe. Wakati wa mazishi yake, mama yake Jane Kasumba aliwalaani wauaji wake imeripotiwa katika magazeti ya Daily Monitor. Amenukuliwa akisema: Nimeumizwa sana, sana. Lakini kinachoniumiza zaidi ...

Read More »

VITUO VIWILI VYA TELEVISHENI YAREJEA HEWANI KENYA

Matangazo ya vituo viwili vya televesheni Kenya, KTN na NTV yamerejea hewani baada ya kufungiwa siku 7 na serikali. Lakini bado haviwezi kutazamwa na Wakenya wengi ambao hawana king’amuzi. Kupitia mtandao wao wa Twitter, NTV wamesema wamerudi hewani kwenye ving’amuzi vya “Dstv, GoTV and Zuku baada ya kufungiwa na serikali.” Stesheni ya iliyokuwa mmojawapo zilizoathirika na hatua ya serikali ,Citizen ...

Read More »

Polisi watumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji Kenya

  Polisi nchini Kenya wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakijaribu kuishinikiza serikali kuvifungua vyombo vitatu vya habari nchini vilivyofungiwa kupeperusha matangazo. “Hii si mara ya kwanza tumiona serikali ya Jubilee ikiangamiza haki za waandishi wa wahabari. Tumeona ikifanyika kwa muda mrefu” Tom Oketch mmojawapo wa waandalizi wa maaandamano hayo ameiambia BBC . “Hawa heshimu sheria, hawa heshumi ...

Read More »

Zuma Agoma Kung’atuka Madarakani

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekataa wito wa chama chake wa kujiuzulu kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo. Rais huyo amekuwa anakabiliwa na shinikizo zaidi kujiuzulu kufuatia mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu katika chama chake cha ANC siku ya Jumapili. Haijafichuliwa mazungumzo hayo yalihusu nini . Bw Zuma aliyefungwa gerezani baada ya kuhsiriki katika vita ...

Read More »

Jacob Zuma Ashinikizwa Kung’atuka Madarakani

Rais wa Afrika kusini anakabiliwa na shinikizo zaidi kujiuzulu kufuatia mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu katika chama chake cha ANC sikuya Jumapili. Haijafichuliwa mazungumzo hayo yalihusu nini lakini viongozi katika chama hicho wanatarajiwa kufanya mkutano wa dharura hii leo Jumatatu. Cyril Ramaphosa aliichukuwa nafasi ya kiongozi wa chama cha ANC kutoka kwa Zuma, anayekabiliwa na tuhuma za rushwa. ...

Read More »

Raia wa Syria Waandamana kupinga Mashambulio ya Uturuki

Maelfu ya watu katika mji uliodhibitiwa na wakurdi Afrin, kakazini mwa Syria wamefanya maandamano kupinga mashambulizi yanaoendeshwa na Uturuki. Uongozi wa ndani wa eneo hilo, wametoa tamko kwa mataifa ya nje kusaidia kusimamisha mapigano hayo, na wameishutumu Urusi kuhusika na yanayoendelea eneo hilo. Ngoma zikipigwa, huku wakibeba mabango yenye ujumbe, waandamani hao wanaonesha hasira walizonazo juu ya kitendo cha uturuki ...

Read More »

ANGELA MERKEL AANZA KUUNDA SERIKALI

NA MTANDAO Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema anakamilisha utaratibu wa kuangalia namna ya kuunda serikali ya mseto kwa kushirikiana na viongozi wa vyama vya Social Democratic na SPD. Amesema wanatarajia kwenda mbele katika jitihada zao za kuunda serikali na ndiyo maana ana matumaini juu ya majadiliano yanayoendelea, huku akisema  anaamini hilo linaweza kufikiwa kwa wakati. Amesema Wajerumani wanahitaji uwepo wa ...

Read More »

RAIS TRUMP AZIDI KUANDAMWA

WASHNGTON, MAREKANI Seneta wa Chama cha Republican nchini Marekani, Jeff Flake, amemkosoa vikali Rais Donald Trump kwa matamshi yake ya mara kwa mara yanayoonekana kuvishambulia vyombo vya habari . Akizungumza katika Baraza la Seneti nchini humo, amesema kiongozi aliyeko madarakani anapokuwa na mazoea ya kutamka matamshi yaliyojaa chembe chembe za kibaguzi kwa watu wengine, ni lazima atakuwa na walakini. Amemkosoa kwa kutumia baadhi ...

Read More »

DAKTARI WA WHITE HOUSE ATHIBITISHA KUWA RAIS TRUMP HANA TATIZO LA AKILI

Rais Trump hajaonyesha dalili zozote za matatizo ya kiakili kufuatia uchunguzi wa kiafya na yuko la afya nzuri, daktari wa White House amesema. “Sina wasi wasi wowote kuhusu afya ya akili ya Trump,” Ronny Jackson alisema Jumanne. Wiki iliyopita Trump alifanyiwa uchunguzi wa afya wa saa tatu, ambao ni wake wa kwanza tangu awe rais wa Marekani. Hii ni baada ...

Read More »

KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI ETHIOPIA AACHIWA HURU

Serikali ya Ethiopia inasema imemuachilia mwanasiasa maarufu wa upinzani baada ya zaidi ya mwaka mmoja kizuizini. Kuachiliwa kwa Merera Gudina mkuu wa chama cha Oromo Federalist Congress, kunafanywa kama sehemu ya jitihada ya kutafuta uwiano wa kitaifa. Siku ya Jumatatu mamlaka zilisema kuwa watafuta makosa kwa wafungwa 500. Pia mamlaka zimehaidi msamaha kuwasamehe wanasiasa kadha wa upinzani walio gerezani na ...

Read More »

MATAMSHI YA TRUMP YASABABISHA BALOZI WAKE KUACHIA NGAZI PANAMA

Balozi wa Marekani nchini Panama amejiuzulu kwa sababu anasema kuwa hawezi tena kuhudumu chini ya utawala wa rais Trump. John Feely ,rubani wa ndege wa jeshi la wanamaji alisema kuwa ilikuwa na heshima kubwa kwake kujiuzulu. Idara ya maswala ya kigeni ambayo inasimamia mabalozi wa Marekani iligundua kwamba amejiuzulu baadaye mwezi Disemba. Kujiuzulu kwake hakukusababishwa na matamshi ya Trump ya ...

Read More »

Umoja wa Afrika Yamtaka Trump Kuomba Radhi kwa Matamshi Yake

Umoja wa Afrika unasema matamshi ya yanayodaiwa kutolewa na rais wa Marekani Donald Trump kuhusu bara la Afrika ni wazi kwamba ni ya ubaguzi wa rangi. Msemaji wa umoja huo , Ebba Kalondo, amesema toni la matamshi hayo lilikera hata zaidi ikikadiriwa idadi ya Waafrika waliouzwa kama watumwa Marekani. Umoja huo unataka rais Trump aombe radhi. Inadaiwa kwamba rais Trump ...

Read More »

Nchi 6 Zinazoongoza Kuwa na Majengo Marefu Duninia

1. Falme za Kiarabu Nafasi ya kwanza inashika na falme za kiarabu ambapo kuna jengo lefu kuliko yote duniani ambalo lipo kwenye jiji Dubai na Linaitwa Burj Khalifa. 2. China Nafasi ya pili inashika na China ambapo kuna jengo lefu linaitwa Shanghai Tower linaloshika nafasi ya pili kwa urefu duniani ambalo linapatika katika jiji la Shanghai China na lina urefu ...

Read More »

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU MELI YENYE BENDERA YA TANZANIA KUKAMATWA UGIRIKI

Serikali imesema inachunguza taarifa za meli yenye bendera ya Tanzania iliyokamatwa nchini ugiriki ikiwa na vifaa vya kutengenezea vilipuzi ambavyo vilikuwa vikisafirishwa kwenda Libya. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Susan kolimba alisema kuwa wanafuatilia kwa kina jambo hilo ili kupata ukweli wake. “Kwa sasa ni kwamba jambo hilo tunalifuatilia ili kujua habari hizo kama ...

Read More »

JAMAA ATUMIA SURURU KUJENGA BARABARA YA KILOMITA 8

Jamaa mmoja katika jimbo lililo mashariki mwa India, amejenga barabara ya umbali wa kilomita 8 akitumia sururu ili kuwawezesha watoto wake kupitia wakitoka shuleni. Jalandhar Nayak, 45, anaishi umbali wa kilomita 10 kutoka shule ambapo watoto wake watatu wa kiume husoma. Lakini safari hiyo huchukua saa tatu kwa sababu vijana hao hulazimika kupitia milima mitano kabla ya kufika nyumbani. Maafisa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons