JESHI la Polisi limemzuia Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kufanya mkutano katika Uwanja wa Mwanga Community Centre  uliokuwa ufanyike jana.

Kwa mujibu wa Barua iliyoandikwa kwa Zitto Kabwe kutoka kwa Mkuu wa Polisi Kigoma Mjini M Mayunga imeelaza kuwa Zitto hakufuata utaratibu uliwekwa na sheria ya Polisi namba 43(1)sura 332 inayomtaka kutoa taarifa ya Mkutano wake ndani ya masaa 48

Barua hiyo imefafanua kwamba Sheria hiyo ya Mwaka 2002 haikufuatwa hivyo akatumia kifungu cha 43(4) kupiga marufuku kufanyika kwa mkutano huo uliokuwa umepangwa kufanyika katika uwanja wa Mwanga manispaa ya Kigoma Ujiji.

Katika Ukurasa wake wa Twitter Zitto Kabwe ameandaika kuwa Polisi wamenizuia kufanya mkutano wangu na wananchi tofati na matakwa ya sharia ya Bunge namba 4(1) inayonipa uhuru wa kufanya mkutano katika jimbo langu.

By Jamhuri