Na Abel Paul

Jeshi la Polisi nchini limetoa tahadhari kwa wananchi wanaotumia vibaya mitaandao ya kijamii hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendela kunyesha ambapo limesema kuanzia Januari hadi Aprili, mwaka huu kumejitokeza matukio ya watoto kufa maji kwa kusombwa na maji maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo watoto 37 wameripotiwa kupoteza maisha.

Akitoa taarifa hiyo leo Aprili 29,2023 msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamisha Msadizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa baadhi ya mikoa ambayo matukio hayo yameripotiwa ni Arusha, Dar es Salaam, Katavi, Kilimanjaro, Kigoma, Morogoro, Mwanza, Pwani na Rukwa.

Misime amebainisha kuwa matukio hayo kuna baadhi ya wazazi wanashindwa kuwalinda watoto wao ambapo amesema Jeshi hilo litaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kushindwa kutekeleza wajibu wa kisheria na kusababisha mtoto kupata madhara.

Sambamba na hilo amesema kuwa Jeshi la Polisi nchini lingependa kutoa tahadhari na onyo kwa wale wachache wanaoendelea kutumia vibaya mitandao ya kijamii na kusababisha hofu,taharuki kwa wananchi.

Pia amesema kuwa kuna taarifa imerushwa hivi majuzi ikionyesha gari Land Cruiser hard top ikisombwa maji ambapo mhalifu aliyetengeneza uongo huo aliandika tukio hilo limetokea muda mfupi huko Arusha ambapo amebainisha kuwa tukio hilo lilitokea mwaka jana nchini Sudan Kusini.

Aidha Misime amesema jamii iendelee kuwakumbusha watumiaji vibaya wa mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya binadamu wenzao wana magonjwa na wanapopata taarifa za kushtua kama hizo wanaweza kupata madhara makubwa zaidi hata kupoteza maisha.

By Jamhuri