Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT ) Wilaya ya Simanjiro Anna Shinini amesema Muungano huo umeendelea kuwaunganisha akina mama Kwa Umoja wao na kuwapa nguvu, ujasiri mkubwa wa kufanya kazi hususani kupitia nafasi ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan kama mwanamke shupavu, Mahili katika kuliongoza Taifa Kama Rais

” Siku ya leo na Mimi kama Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Simanjiro namuunga mkono mama yetu Mchapakazi Mh. Samia Suluhu Hassan ambaye ni mwanamke aliyetujengea ujasiri mkubwa na sisi tunamuumga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kumtia moyo katika Utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku, amesema Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Simanjiro

Aidha Shinini amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha mikopo ya asilimia 10 iliyokua ikitolewa katika kila Halmashauri hapa Nchini kupitia mapato yake ya ndani, ni mikopo iliyokuwa na msaada mkubwa sana kwa walengwa katika kuwaondoa katika wimbi la u amaskini na kuwainua kiuchumi.

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara Anna Shinini

” Nimefurahi sana leo kusikia ile mikopo ya asilimia 10 imerudi, kwani ilikua ndio nguzo muhimu ya kumkomboa mwanamke, vijana na Watu wenye ulemavu na hatimaye kuwakomboa kwenye wimbi la umaskini, kwani mikopo ya nje ya Serikali baadhi imekua ni mikopo kandamizi Kwa kuwa na riba kubwa iliyowapelekea hata baadhi yao kufilisiwa mali zao kwa kushindwa kurejesha marejesho.

Aisha SHININI amesema Mikopo hii ilishakuwepo ambapo Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu walikua wakinufaika nayo kwani Serikali imekua ikitoka mikopo hiyo hiyo bila riba ili kuwawezesha kuinua uchumi na hivyo kuwawiaburahisi kuwaletea Maendeleo ya haraka, ukilinganisha na hiyo mikopo mingine.

” Sasa wanaendelea kupata mikopo, tunamshuku sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha mikopo hii ambayo itawasaidia kuwainua kiuchumi na hatimaye kuweza kuondokana na umaskini, kikubwa ni umaminifu wa kuchukua fedha na kurudisha”

Kufuatia hilo pia amewataka wanaochukua mikopo kuweza kuhakikisha mikopo wanayoichukua inawanufaisha kisawa sawa ikiwa ni sambamba na kurudisha fedha hizo Kwa wakati ili iliwe kuwasaidia na wengine

Aidha amewataka wanawake pamoja na wananchi wote Kwa ujumla kuhakikisha wanamuunga mama mkono kwasababu Muungano wetu ni kioo, ni dira ndani ya nchi yetu ndio inayotuonyesha tumetoka wapi, tuko wapi na tunatarajia kufika wapi, na hivyo Rais Samia anatupa nguvu zaidi kuweza kufanya kazi ndani ya Taifa letu.