Na Aziza Nangwa, Jamhuri Media, Zanzibar

Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Vijana Duniani, Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO) limedai vijana ni nguvu ya leo, wajibu wa kesho na walinzi wa dunia, hivyo wanapaswa kupewa nafasi na mazingira rafiki ya kushiriki katika maendeleo ya jamii.

Rai hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu TRAMEPRO, Bonventura Mwalongo ambapo amesema siri kubwa ya mafanikio ya taifa ni kuwawezesha vijana kutumia uwezo, elimu, vipaji na ubunifu wao katika kutatua changamoto zinazolikabili taifa na dunia kwa ujumla.

Mwalongo amesema , vijana wana nafasi kubwa na muhimu katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa mazingira, ukosefu wa ajira pamoja na matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali za asili.

Amesema vijana wanatakiwa kutumia teknolojia na ubunifu kuanzisha shughuli za uzalishaji zitakazoongeza ajira na kipato huku
zikizingatia utunzaji wa mazingira.

Pia amesisitiza umuhimu wa elimu ya mazingira kwa vijana ili wawe kuwa sehemu ya kutafuta suluhisho la changamoto zinazolikabili jamii.

Mwalongo amesema wazazi, taasisi za elimu, serikali na sekta binafsi kushirikiana kuwaandaa vijana kwa kuwapatia elimu, maarifa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya sasa ya jamii na uchumi.

Amedai kuna umuhimu wa kuwashirikisha vijana katika maamuzi yanayohusu maendeleo yao na mustakabali wa nchi,kwa kuwa
ushirikishwaji huo unaweza kuongeza uwajibikaji, ubunifu na uzalendo miongoni mwa vijana.

”Siku ya Vijana Duniani hutumika kuwakumbusha jamii kuhusu nafasi muhimu ya vijana katika maendeleo, huku ikisisitiza haja ya kujenga mazingira yatakayowawezesha kutumia nguvu na vipaji vyao kwa manufaa ya jamii.

Tunasema uwekezaji kwa vijana ni uwekezaji wa taifa la kesho, hivyo serikali, taasisi na jamii kwa ujumla wanapaswa kuweka mikakati ya kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika maendeleo endelevu.

Taifa linalowekeza katika vijana linaweka msingi wa maendeleo imara, ubunifu na ulinzi wa mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo, Afrika hazina uhaba wa vijana”amesema

Amesema uwekezaji sahihi kwa vijana hatuhitaji wanaosubiri maisha yabadilike. tunahitaji vijana wanaobadilisha maisha kwa kutukia fursa zilizopo.

Mwalongo ametoa wito wa kujenga mkataba mpya wa kizazi kati ya vijana, Serikali, jamii, wazee, viongozi wa dini,watafiti, sekta
binafsi na mashirika ya kiraia.

Mkataba huo ujengwe juu ya misingi ya elimu, afya, ajira, sayansi,teknolojia, maadili, tiba asilia, bioanuwai, mazingira, amani namaendeleo endelevu,kwani Tanzania na