Na Isri Mohamed

Klabu ya soka ya Simba leo Aprili 28, 2024 imetangaza rasmi kuachana na kocha wake Mkuu, Abdelhak Benchika na wasaidizi wake wawili kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Benchika alijiunga na Simba mwezi Novemba mwaka jana, na amefanikiwa kutwaa Makombe mawili la ngao ya jamii na la Muungano waliloshinda jana visiwani Zanzibar.