
Nashauri Aisha apewe tuzo ya kitaifa
Laiti tungekuwa tunahangaishwa na mambo serious, kwa hakika taarifa ya dada Aisha Twalibu, mlinzi wa kampuni binafsi pale Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, ndiyo ingepamba mijadala kwenye vyombo vya habari na mitaani kwetu kote. Huhitaji kuelezwa ukweli kwamba mtu yeyote anayefanya kazi ya lindo kama alivyo Aisha ni mtu mwenye maisha ya kawaida mno. Huwezi kumpata…