Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia, Dar es Salaam
Chama cha ACT Wazalendo kimeishauri Serikali kufanya ukaguzi na ukarabati wa miundombinu ya maji ikiwemo mita, mabomba, matanki, ili kuzuia upotevu wa maji na kudhibiti mifumo ya maji taka yanayovuja ovyo hali itakayopelekea wananchi kuugua magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Ameyasema hayo leo Mei 10, 2024 Waziri kivuli wa chama cha ACT Wazalendo Wizara ya maji Yasinta Awati akichambua makadirio ya mapato ya na matumizi ya bajeti kwa mwaka 2024/2025 ambapo wameidhinishiwa shilingi bilion 627.77 huku shilingi bilioni 69.66 ambapo shilingi bilioni 69.66 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 558.11 kwa ajili ya Miradi ya maendeleo iliyowasilishwa jana bungeni na Waziri wa Maji Jumaa Aweso.
Waziri Kivuli ACT Yasinta amesema bajeti hiyo ni pungufu kwa shilingi bilioni 128.5 sawa na 17% ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana 2023/2024. ACT Wazalendo kupitia baraza kivuli la Mawaziri wameisoma na kuichambua bajeti hiyo ili kuona kama itaenda kutatua changamoto za sugu zinazoikabili sekta ya maji nchini .
“Kwa hakika katika uchambuzi wetu wa bajeti hii 2024/25 na utekelezaji wa bajeti iliyopita ni wazi kuwa uzembe, ubadhirifu na kutowajibika kwa viongozi kunaendelea kulifanya taifa kukosa huduma bora za maji” amesema Yasinta.
Hata hivyo amebainisha kuwa mwenendo wa bajeti kushuka kunaonesha kuwa kero na matatizo kuhusu huduma za maji mijini na vijijini itaendelea kuwepo kwa miongo kadhaa mbele kwani kasi ndogo ya usambazaji na upatikanaji duni wa maji Mijini na Vijijini imekuwa ikiliezwa na Mahitaji ya maji kwa umma yanaongezeka kwa asilimia 7 kila mwaka, lakini uzalishaji wa maji umeongezeka kwa asilimian2.6 kwa mwaka 2024/25.
Sababu kubwa ya uzalishaji kuwa chini ni uwezo mdogo wa Wizara ya Maji kusimamia miradi mbalimbali ya maji na ufinyu wa bajeti na kupelekea. miradi mingi ya maji kutokamilika kabisa au kuzalisha kiwango kidogo cha maji.
“Kwa mwaka wa fedha wa 2024/25 uzalishaji wa maji nchini ni asilimia 58 tu ya uhitaji wa maji wa wananchi, hivyo kusababisha tatizo la upatikanaji wa maji au tatizo la mgawo na kupelekea wananchi kutumia muda mwingi na gharama kubwa kutafuta maji hali ya upatikanaji wa huduma za maji safi na salama vijijini ni asilimia 79.6 tu asilimia hizo zinatajwa kwa maana miradi iliyofika sio upatikanaji wa huduma ya maji.
Taarifa ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS 2023) inaonyesha miradi ya maji iliyowekezwa vijijini takribani asilimia 38 haifanyi kazi kwa ufanisi au imekoma kabisa kutoa huduma na zaidi ya vijiji 497 nchini Tanzania havijafikiwa na mradi wowote wa maji” amesema Waziri Kivuli
Waziri huyo amebainisha kuwa kutokamilika kwa muda mrefu kwa Mradi wa Maji wa Kagongwa – Isaka kwenda katika Vijiji vya Mwalugulu, Kilimbu, , Butondolo na Itogwanholo, mradi wa maji Ruangwa – Nachingwea, Mkinga – Horohoro, Morunganya – Morogoro Vijijini, Ukiliguru, Sumve hadi Koromije ni miongoni mwa miradi ambayo kama ingekamilika kwa wakati ingepunguza uhaba wa upatikanaji wa maji kwa wanavijiji .
Aidha Wizara isimamie uwajibikaji wa Mamlaka hizo na kuwachukulia hatua watendaji na wasimamizi wanaozembea katika kuhakikisha upatinaji wa uhakika wa maji kwa wananchi kwani hiyo tabia imekuwa mwendelezo wa uzembe na ubadhirifu wa fedha za miradi ya Maji.
“Kumekuwa na wimbi kubwa sana la ubadhirifu wa fedha za miradi ya maji inayopelekea ucheleweshwaji wa upatikanaji wa huduma za maji katika maeneo husika. Kila mwaka wa ukaguzi wa matumizi ya fedha zinazoidhinishwa na Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali, wizara hii imekuwa ikikutwa na hoja zenye thamani ya mabilioni ya Shilingi zilizotafunwa sasa miaka mitatu mfululizo Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeonesha ubadhilifu; Ripoti ya mwaka 2020/21 ilionyesha kulikuwa na fedha kiasi cha shilingi bilioni 37.1 na dola za kimarekani milioni 6.05 ” amesema Waziri kivuli
Vilevile kuna ombwe kubwa sana katika bei za kuunganishwa na huduma ya maji. mpaka sasa hakuna bei elekezi ya kuunganishwa na huduma ya maji nchini hivyo wananchi wanalipa fedha nyingi katika kuunganishwa na huduma hiyo, wakati kuna huduma ya kuunganishiwa Umeme vijijini na bei elekezi kwa huduma hiyo ni shilingi 27,000 kwanini Huduma ya maji haina mfumo huo kiasi watu wanalazimika kulipa mpaka 300,000.
Jambo jengine ni kukithiri kubambikiwa bili, wananchi maeneo mbalimbali wamekua na malamiko ya kubambikiwa bili na kulipishwa zaidi ya matumizi yao, mara nyingi ni kutokana na ubovu wa Dira, mkataba wa huduma kwa wateja unataka mteja anapolalamika dira irekebishwe ndani ya siku 7 dira irekebishwe au ibadilishwe, lakini haifanyiki hivyo hivyo ukaguzi wa mfumo wa mita za malipo ya kabla, na serikali kugharamia mita hizo kuwafungia wananchi ambao wanalipia huduma za maji.
Aidha chama cha ACT kimetoa wito kwa Serika itangaze bei elekezi na nafuu ya kuunganishwa na huduma ya maji mijini na vijijini ili iwe rahisi wananchi kuvuta maji majumbani mwao na wakicheleweshewa walipwe fidia