Mkurugenzi wa huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amekerwa na kitendo cha uhifadhi damu kwenye jokofu la matumizi nyumbani .

Hayo yamebainika katika Hospitali ya halmashauri ya mji Korogwe Magunga wakati wa ziara mkoani humo.

Dkt. Mfaume ameonesha kukerwa na kutoridhishwa na kitendo hicho na kuelekeza kufanyika utaratibu wa haraka wa upatikanaji ya jokofu maalumu kwa kuhifadia damu.

“Hili jokofu ambalo mnatunzia damu ni kama tulilolikuta kule na hii tumeletewa na mdau lakini ni jokofu ambalo aliyetengeneza pale chini ‘fresh vegetables’ yaani mbogamboga kama mchicha tumetoka kule Shinyanga Mwalugulu tumewasema tukajua huku mmejifunza mtahangaika na sisi hatutaki kuona haya yanayofanyika huku tuyaone sehemu nyingine lakini mnaonekana Korogwe TC mnawataalamu wa kununua domestic fliji na kuhifadhi maabara tumeenda tumekuta majokofu sita jumla Domestic” amesema Dkt. Mfaume.

Ikumbukwe Aprili 2024 wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika Mkoa wa Shinyanga timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI ilibaini ukiukwaji ma manunuzi ya majokofu ya kuhifadhia damu katika kituo cha afya Mwalugulu kilichopo halmashauri ya Msalala.

By Jamhuri