Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa wito huo kwa Viongozi na Watendaji wa Ushirika kutumia Dhamana hiyo waliyopewa kwa Uaminifu na Weledi Mkubwa

RC Chalamila ameyasema hayo Jana katika ufunguzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Dar es Salaam lililofanyika katika Ukumbi wa Blue Sapphire- Mbezi Beach Dar es Salaam.

Chalamila amesema ili Ushirika uzidi kukua na kuimalika unapaswa kuwa na Umoja, Kiasi, Umakini, Maadili, na Itikadi.

Aidhaa, Mkuu wa Mkoa amesema kwa kuwa Ushirika ni Ushirikiano ulio salama zaidi kwa kuwa unadhibitiwa na Serikali hivyo ni vema Waajiri kupeleke makato ya wanachama wao kwenye Saccos ili yaweze kutekelezwa kwa wakati.

Vile vile RC Chalamila amewataka Viongozi kuhamasisha matumizi ya kidigitali ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji pamoja na Mamlaka za kiusimamizi sambamba na kuongeza ushirikiano wa kibiashara wao kwa wao katika Mikopo na Masoko.

Kwa upandea wake Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni Saad Mtambule amewataka Wanaushirika kuhamasisha zaidi kwenye Weledi, Juhudi na Uwekezaji.

Naye Anjela Nalimi ambaye ni Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Dar es Salaam amesema Ushirika unaendelea kutoa mchango Mkubwa katika uchumi wetu katika nyanja za Mitaji, Ajira, Masoko, Uzalishaji, Makazi na Kadhalika.

By Jamhuri