Watu 72 wamekufa kwa kuzama kwenye maji tangu mwanzo mwa mwezi huu, huku rekodi ikionesha vifo vingi zaidi vimetokea katika kipindi hiki cha mapumnziko ya siku za Sikukuu ya Pasaka.

Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Polisi la Ufilipino, Kanali Jean Fajardo, rekodi ya vifo 67 inajumuisha matukio ya kuanzia Aprili Mosi hadi Jumapili ya Pasaka, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Amesema watu wengi walifurahishwa na kutembelea maeneo mazuri ya fukwe, huku baadhi ya vifo vilihusisha watoto walioachwa bila ya uangalizi, vingine ulevi na wengine mikasa ya kusukumana wenyewe kwa wenyewe kwenye maji.

Vifo vitokanavyo na kuzama kwenye maji vinachukua nafasi ya tatu duniani. Shirika la Afya Duniani linakadiria watu 236,000 wanakufa kila mwaka duniani kutokana na mikasa hiyo.

By Jamhuri