Zaidi ya watu 140 wamefariki dunia nchini Pakistan baada ya kupigwa na radi na matukio mengine yanayohusishwa na dhoruba katika mwezi huu wa Aprili, huku taifa hilo likishuhudia mvua kubwa kabisa.

Pakistan imekumbwa na mafuriko makubwa, maporomoko ya ardhi na hali mbaya ya hewa iliyosababisha nyumba kadhaa kubomoka huku katika baadhi ya maeneo kukiwa na uharibifu mkubwa wa mazao.

Msemaji wa Idara ya Hali ya Hewa nchini humo, Zaheer Ahmad Babar, amesema taifa hilo limeshuhudia mvua yenye “ongezeko la asilimia 164” ikiwa ni juu ya viwango vya kawaida katika mwezi huu wa Aprili.

Mnamo mwaka 2022, theluthi moja ya Pakistan ilifunikwa na maji kufuatia mvua kubwa kuwahi kushuhudiwa zilizosababisha mamilioni ya watu kuhama makaazi yao.

Benki ya Dunia inakadiria kuwa taifa hilo lilipata hasara ya dola bilioni 30 kutokana na mvua hizo.

Please follow and like us:
Pin Share