Author Archives: Jamhuri

Marekebisho vitambulisho vya wamachinga yanahitajika

Rais John Magufuli amejipambanua kama kiongozi mpenda wanyonge. Mara zote amesikika na hata ameonekana akiwatetea watu wa kada hiyo ambao kwa muda mrefu wametaabika. Hili ni jambo jema linalostahili kutendwa na kiongozi mkuu wa nchi. Katika kutekeleza dhana hiyo ya kuwa “Rais wa Wanyonge”, amehakikisha kodi nyingi zilizokuwa kero kwao zinaondoshwa. Akaona hiyo haitoshi. Akaandaa vitambulisho vya wachuuzi kwa kuwatoza ...

Read More »

Wananchi tunataka mabadiliko

Siasa ni sayansi, ni taaluma pia. Sayansi ina ukweli na uhakika, na taaluma ina maadili, kanuni na taratibu zake. Siasa ni mfumo, mtindo, utaratibu au mwelekeo wa jamii katika fani zake zote za maisha. Ni utaratibu uliowekwa au unaokusudiwa kuwekwa na chama kinachoongoza nchi, au kinachokusudia hivyo ili kukiwezesha chama hicho kunyakua au kudumisha uongozi wake. Mtu aliyomo katika taaluma ...

Read More »

Yah: Tumemaliza AFCON tujipange

Nianze kwa kuwapongeza vijana ambao kwa mara ya kwanza wametambua kwamba ni wawakilishi kwa maana ya mabalozi wetu waliokuwa wakipigania mafanikio ya taifa. Nawapongeza sana na tumeona ni jinsi gani ambavyo pamoja na jitihada zote kubwa walizokuwa nazo tumeshindwa kufanikiwa kuendelea kupeperusha bendera yetu kimataifa. Si jambo baya kwa sasa kwa kuwa bado tu wachanga katika vita ambayo wengine wameizoea ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (5)

Wiki iliyopita katika sehemu ya nne hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Akina mwewe pia walikuwepo wananyakua matambara kwa fujo kisha wanalia Zwi! Zululu! Ndege wengine wadogo walikuwa wanaruka juu juu na baadhi yao walikuwa wanaruka chini chini. Bata mzinga nao pia walikuwa wanahimiza wakisema mrudisheni mtoto wetu jamani, mrudisheni kwani amepotea na tunamtafuta.” Je, unafahamu nini kinafuata? Endelea… Bulongo, ndoto ...

Read More »

V.MONEY unakua kimuziki na kuikuza sanaa yako

Sikio halilali njaa, wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva baada ya kukanyaga na kutimua vumbi mitaani kwa nyimbo za vijana wa kundi la Wasafi (WCB) sasa ni muda wa Vanessa Mdee, maarufu kama Cash Madame na wimbo wake wa ‘Moyo’. Vanessa Mdee ambaye kwa mashabiki wake anafahamika zaidi kama V. Money, ameachia wimbo wa ‘Moyo’ wiki iliyopita ukiwa ni sehemu ...

Read More »

Lampard kuanza kipimo na vigogo

Wiki iliyopita mchezaji wa zamani wa timu ya Chelsea na West Ham United, Frank Lampard, alitangazwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Chelsea (The Blues). Timu hiyo inayopatikana katika Jiji la London, Uingereza, imeingia mkataba wa miaka mitatu na Lampard ambaye kabla ya mkataba wake huo wa kuinoa Chelsea alikuwa kocha wa Derby Country, klabu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza England. Lampard ...

Read More »

Bomu la ardhi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amepata jaribio kubwa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. “Siku moja baada ya kuingia ofisini, alijifungia ofisini kwake akasema ana shughuli nyingi hivyo asingeweza kumwona mtu yeyote. Ghafla, akaja mzee mmoja. Akamweleza msaidizi wake tukio la kusikitisha. Tukio lenyewe lilikuwa kama sinema vile. ...

Read More »

Bibi mjane Dar amlilia Makonda

Serikali ya Mtaa wa Nzasa Somelo, Kata ya Zingiziwa, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imetumia hila kumnyang’anya shamba la ekari tatu bibi mjane mwenye umri wa miaka zaidi ya 70. Shamba hilo ambalo limetenganishwa na Mto Nzasa, kipande kimoja kikiwa Wilaya ya Kisarawe na kingine Wilaya ya Ilala ni miliki ya Theresia Vingambudi ambaye anaishi Halmashauri ya Kisarawe, ...

Read More »

Olduvai: Bustani ya ‘Eden’

Julai 17, 1959 Mary Leakey aligundua fuvu katika eneo linaloitwa FLK-zinj katika Bonde la Olduvai, Ngorongoro mkoani Arusha. Lilikuwa fuvu la zamadamu wa jamii ngeni, hivyo yeye na mume wake Louis Leakey waliita Zinjanthropus boisei. Hapa ndipo mahali kunakotambulika duniani kote kuwa ndiko kwenye asili ya binadamu. Kutoka hapa binadamu walisambaa katika sayari yote ya dunia. Mamia kwa mamia ya ...

Read More »

Sheria ya Takwimu funzo

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekamilisha mkutano wake wa bajeti wiki iliyopita. Ukiondoa mjadala wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020, masuala mengine kadhaa yalijitokeza bungeni. Mojawapo ya mambo hayo ni serikali kuwasilisha mabadiliko ya sheria ya takwimu, marekebisho yaliyolenga vifungu vya sheria hiyo kuhusu haki ya kuchapisha au kutoa taarifa za takwimu kwa umma. Mabadiliko ...

Read More »

NINA NDOTO (24)

Watu ni mtaji   Siku, wiki, miezi, miaka vinapita mbele yangu mimi kwanini nisimshukuru Mungu kwa kunilinda vyema? Nasema asante Mungu kwa zawadi ya Maisha. Naandika makala hii nikiwa na furaha sana kwa kufikisha mwaka mwingine. Ni furaha iliyoje. Asante Mungu kwa mara nyingine. Wanasema kushukuru ni kuomba tena. Tangu zamani ndoto yangu ilikuwa ni kuandika vitabu na kuwahamasisha watu. ...

Read More »

Wadaiwa sugu KCBL waanza kusakwa

Benki ya Ushirika mkoani Kilimanjaro (KCBL) imeanza msako dhidi ya watu binafsi, vikundi vya wajasiriamali na kampuni zinazodaiwa mikopo na benki hiyo baada ya kushindwa kufanya marejesho ndani ya muda kulingana na masharti ya mikopo. Msako huo unafanywa na benki hiyo kupitia Kampuni ya Tanfin Consultant E.A Ltd ya jijini Dodoma ambayo imepewa ridhaa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (20)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa kuwasisitiza wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni kuhakikisha wanafunga hesabu zilizokaguliwa na kuziwasilisha TRA. Ni imani yangu kuwa wengi kama si nyote mlitekeleza na kama hukufanya hivyo, wasiliana haraka na ofisi ya TRA iliyopo karibu yako, kwani bila kufanya hivyo unahatarisha uhai wa kampuni yako kwa faini za kisheria. Sitanii, nichukue fursa hii kulishukuru Baraza ...

Read More »

Rostam: Wafanyabiashara tuzingatie sheria

Yafuatayo ni maelezo ya mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, wakati wa uzinduzi wa kampuni ya utoaji huduma za gesi, Taifa Gas, anayoimiliki. Katika kampuni hiyo, Rostam ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Uzinduzi huo ulifanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wiki iliyopita, Kigamboni, jijini Dar es Salaam. “Mheshimiwa Rais, waheshimiwa mawaziri, mheshimiwa mkuu wa ...

Read More »

JAMHURI kinara tena

Gazeti la uchunguzi la JAMHURI limetwaa tuzo mbili za uandishi bora wa habari (Excellence in Journalism Awards Tanzania – EJAT) kwa mwaka 2018, tuzo zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Hatua hiyo ni sehemu tu ya mafanikio ya gazeti hilo ambalo mwaka jana liliongoza dhidi ya vyombo vingine vyote vya habari Tanzania Bara na Zanzibar vilivyohusishwa kwenye utafiti wa ...

Read More »

Tunaihitaji sekta binafsi – Rais Dk. Magufuli

Kwa hiyo sekta binafsi endeleeni kujiamini, endeleeni kufanya kazi, mje Tanzania hapa ni mahali salama kwa uwekezaji. Tunawahitaji leo, tuliwahitaji juzi, tutawahitaji keshokutwa, tutawahitaji miaka yote kwa sababu Tanzania iko hapa kwa miaka yote. Tangu leo, kesho, keshokutwa na maisha yote.” Ifuatayo ni sehemu ya maneno kutoka katika hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ...

Read More »

Ndugu Rais, anayejidhania amesimama aangalie asianguke

Ndugu Rais, kama wapo wenzetu waliodhani kuzuia Bunge kuonekana kwa wananchi moja kwa moja kutawafanya wasijue yanayofanyika ndani ya Bunge, sasa wakiri kuwa hawakufikiri sawa sawa. Lisiporekebishwa hili kabla ya uchaguzi mkuu ujao itakuwa ni kwa hasara yetu wenyewe! Udhaifu wa Bunge katika sakata la CAG, timamu gani hakuuona? Baada ya kijana wetu mahiri Stephen Masele kujitetea Bunge lilioga fedheha ...

Read More »

TPA: Usalama ni namba moja katika shughuli za bandari

Bandari ni lango la biashara kitaifa na kimataifa, hivyo ni muhimu sana kufanya biashara katika bandari zenye usalama na mazingira rafiki na yanayovutia wateja. Kwa hiyo TPA ina wajibu wa kuhakikisha bandari zote nchini ni salama kwa wafanyakazi ili waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki na salama kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi. Pia TPA ina wajibu wa kuweka mazingira ...

Read More »

Tumechimba kaburi la utalii wa filamu

Hapa Tanzania ukitamka neno ‘utalii’, haraka haraka akili za watu hukimbilia kwenye mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro labda na fukwe za Zanzibar: Basi! Hata serikali inaelekea kufikiria hivyo, ndiyo maana mkazo kuhusu utalii uko kwenye aina hiyo tu ya utalii. Namna hii finyu ya kuuangalia utalii ndiyo inayosababisha tuwe na watalii wachache licha ya kuwa na vivutio vingi nadra na ...

Read More »

Mali iliyopatikana kabla ya ndoa inahesabika ya familia?

Mara kadhaa linapoibuka suala la kugawana mali pale ndoa inapohesabika kushindikana, masuala kadhaa ya msingi na yanayohitaji uelewa huwa yanaibuka. Moja ya suala kati ya masuala ambayo huibuka ni hili la kutenganisha na kufafanua hadhi ya mali za wanandoa ili mgawanyo uweze kufanyika kwa haki. Yawezekana mwanandoa akadhani ana haki katika mali fulani lakini kumbe kisheria hana haki hiyo, ni mtazamo wake ndio ...

Read More »

Uponyaji wa majeraha katika maisha (2)

Katika familia yangu tuliwahi kupata jeraha. Septemba 14, 1999 lilitokea tukio la kuhuzunisha kwenye familia yangu. Dada yangu kipenzi, Cecilia aliuawa kikatili, na aliyetenda tukio hilo ni mumewe. Dada aliuawa akiwa anamnyonyesha mtoto wake wa kike aliyekuwa na umri wa miezi mitano. Tukio hili tulilipokea kwa mwono wa dharau. Tuliamini kwamba, mume wa dada yetu amemuua dada yetu kwa kutudharau. ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (35)

Simba akizidiwa hula nyasi, huchambua asile miiba   Kutekeleza maono ni mtihani. Maono ni kuona ambacho hakionekani.  Kuna aliyesema: “Mtu bila maono ni mtu bila wakati ujao. Mtu bila wakati ujao atageukia wakati uliopita.” Atausifia wakati uliopita. Kuna wajenzi watatu waliokuwa wanajenga ukuta. Mpita njia alimuuliza wa kwanza, mnafanya nini? Alijibu: “Tunapanga matofali.” Alimuuliza wa pili, mnafanya nini? Alijibu: “Tunajenga ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons