Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera imefanikisha kuongeza wigo wa mtandao wa barabara ambapo jumla ya Km 108 za barabara mpya ambazo hazikuwepo kabisa zimefunguliwa.

Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Karagwe, Mhandisi Simon Mhina alipozungumzia mafanikio ya Miaka Mitatu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Bajeti ya TARURA imeongezeka kutoka Shilingi Bil. 1.72 katika mwaka wa fedha 2020/21 hadi Shilingi Bil. 8.269 mwaka wa fedha 2023/2024,” alisema.

“Tunamshukuru Rais Samia kwani ongezeko hili la bajeti limewezesha ujenzi wa barabara mpya maeneo yaliyokuwa awali hayafikiki kabisa”.Ameongeza

Amebainisha pia barabara za changarawe zimeongezeka kutoka Km 515.03 hadi Km 847, barabara za lami kutoka Km 10.85 hadi Km 25.12 na barabara za udongo zimepungua kutoka Km 514.98 hadi Km 403.66.

Mhandisi Mhina alisema pamoja na hayo pia wameweza kufanikisha ujenzi wa makalavati mapya 208.

By Jamhuri