Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Dustan Kyobya na Mkurugenzi wa Ifakara Mji Zahara Michuzi , wamefika eneo la kingo za mto Lumemo ambao umejaa sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuleta mafuriko kwenye makazi na taasisi za umma na binafsi.

Mkuu wa wilaya amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema na kuondoka maeneo yote yaliyojaa maji.

Baadhi ya shule zimelazimika kufungwa kwa muda mpaka maji yatakapopungua

Timu za uokoaji zimepata boti kutoka TAWA na zinaendelea na doria ya nyumba kwa nyumba kuokoa wananchi.

Nyumba nyingi bado zimezungukwa na maji, hivyo timu za uokoaji zikiongozwa na Kamanda wa Zimamoto wilaya kamanda Haji , Skauti wilaya, Redcross wilaya na Halmashauri zinaendelea na doria za nyumba kwa nyumba kuokoa wananchi walioshindwa kutoka majumbani mwao    

Please follow and like us:
Pin Share