Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Mbeya

Serikali imewaondolewa mzigo wakulima baada ya kuzinduliwa kwa Mpango wa Ruzuku ya Mbolea utakaowawezesha kupata nafuu ya bei za mbolea katika msimu wa kilimo 2022/2023.

Uzinduzi huo umefanywa leo Agosti 8, 2022 na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima Nanenane inayoadhimishwa kitaifa mkoani Mbeya.

Waziri wa Kilimo Hussen Bashe amesema mpango huo unalenga kuwaondolea mzigo wakulima ambao wamekuwa wakikutana nao kwa muda mrefu kutokana na changamoto za bei za mbolea.

Mpango huo wa rukuzu unafanya bei ya mbolea ya DAP kuuzwa Sh70, 000 kutoka Sh131,000 ya awali huku mbolea ya urea ikiuzwa Sh70,000 kutoka Sh124,734.

By Jamhuri