Tag Archives: mafanikio

Mafanikio yoyote yana sababu (24)

Padre Dk Faustin Kamugisha Kuwajali wateja ni sababu ya mafanikio. Mteja ni kama damu muhimu kwa uhai wa biashara yako au shughuli yako. Kanuni ya msingi kwa yeyote anayehudumia mteja ni mteja kwanza. Mteja ni mfalme. Inaweza kukuchukua miezi kumpata mteja na sekunde moja kumpoteza. Usipowajali wateja wako, mtu mwingine atawajali. Yatafakari maneno ya Mahatma Gandhi: “Mteja ni mgeni muhimu ...

Read More »

Mafanikio yoyote yana sababu (20)

Mafanikio yoyote yana sababu (20) Padre Dk Faustin Kamugisha Kutenda au kuchukua hatua ni siri ya mafanikio.  Ahadi ni wingu, kutenda ni mvua. Ni methali ya Kiarabu. “Kutenda ni ufunguo wa msingi wa mafanikio yote,” alisema Pablo Picasso (1881-1973), mwandishi wa maigizo, mpaka rangi na mchongaji wa sanamu wa Hispania. Matendo yana kauli kuliko maneno. Watu wanaofaulu wanafika juu ya mlima kwa ...

Read More »

MAFANIKIO YOYOTE YANA SABABU (19a)

Padre Dk Faustin Kamugisha Uvumilivu au ustahimilivu ni siri ya mafanikio. Uvumilivu ni kuanguka mara 99 na kuinuka mara ya 100. Katika msingi huu Julie Andrews alisema, “Uvumilivu ni kushindwa mara 19 na kushinda mara ya 20.” Matone yanayodondoka mwishowe humomonyoa mwamba. Ni methali ya China. “Kama Columbus angerudi alikotoka, hakuna mtu yeyote ambaye angemlaumu. Lakini hata hakuna mtu yeyote ...

Read More »

Mafanikio yoyote yana sababu (14)

Na Padre Dk. Faustin Kamugisha   Kuwa na ndoto na kuzifanyia kazi ni siri ya mafanikio. Watu wanaofanya vitu vikubwa wanaota ndoto kubwa. Watu wanaofanya vitu vingi sana wanaota ndoto nyingi sana.   “Unaamini katika ndoto? Ukitaka ndoto zako ziwe ukweli wa mambo usipitilize katika kulala! Usiache ndoto ziwe jinamizi,” alisema Henrietta C. Mears (1890–1963) mwelimishaji.   Kuwa na ndoto ...

Read More »

Mafanikio yoyote yana sababu (11)

Na Padre Dk. Faustin Kamugisha   Shukrani ni sababu ya mafanikio. “Kama unataka kugeuza maisha yako, jaribu kushukuru. Maisha yako yatabadilika kwa kiasi kikubwa sana,” alisema Gerald Good. Ingawa tuna mioyo midogo, lakini inaweza kubeba jambo kubwa nalo ni shukrani. Hesabu mafanikio usihesabu matatizo. Hesabu baraka, usihesabu balaa. “Afadhali kupoteza hesabu wakati unahesabu baraka zako kuliko kupoteza baraka wakati unahesabu matatizo yako,” alisema ...

Read More »

Mafanikio Yoyote Yana Sababu (9)

Na Padre Dk Faustin Kamugisha   Nia ni sababu ya mafanikio. Penye nia pana njia. Mtazamo wa “lazima nifanye kitu,” unatatua matatizo mengi kuliko mtazamo wa “kitu fulani lazima kifanyike.” Mtazamo wa kwanza una nguvu ya nia. “Nia yetu inaumba uhalisia wetu,” aliandika Wayner Dyer katika kitabu chake The Power of Intention. Yote ambayo umeyafanya kuna wakati uliyanuia. Mambo mengi ...

Read More »

MAFANIKIO YANA SABABU YOYOTE (7)

Na Padre Dkt. Faustin Kamugisha Mtazamo chanya ni sababu ya mafanikio. Mtazamo chanya unakufanya uyaone matatizo kuwa ni baraka katika sura ya balaa. Mtazamo chanya unakufanya kuhesabu siku zako kwa saa za furaha na si kwa saa za karaha. Mwenye mtazamo chanya akijikuta katika maji anaamua kuoga. Washindi wengi wana mtazamo chanya. Kuna aliyesema “Mshindi kila mara ni sehemu ya ...

Read More »

MAFANIKIO YOYOTE YANA SABABU (6)

Padre Dk Faustin Kamugisha Kushindwa ni sababu ya mafanikio ilmradi kusiwe desturi. Bill Gates, tajiri mkubwa duniani, amesema, “Ni vizuri kusherehekea mafanikio, lakini ni muhimu kujifunza masomo unayopewa na kushindwa.” Kushindwa huwafanya baadhi ya watu kuvunjika moyo na wengine kuvunja rekodi baadaye. Ndugu msomaji, umeshindwa mara nyingi ingawa huwezi kukumbuka. Ulishindwa mara ya kwanza ulipojaribu kusimama. Ulishindwa mara ya kwanza ...

Read More »

Mafanikio Yoyote Yana Sababu (2)

Kufikiria vizuri ni sababu ya mafanikio. Tazama mbele ufikiri. Papa Fransisko alisema kuna lugha tatu: ya kwanza fikiria vizuri, ya pili hisi vizuri, ya tatu tenda vizuri.  Kufikiria vizuri ni msingi wa mafanikio. Kuna aina mbalimbali za kufikiri. Kwanza ni kufikiria kwa ‘kufokasi’. Fokasi ni mahali miale ya nuru ikutanapo. Kuwa makini na lengo lako. Mambo ambayo si muhimu yanayokuondoa ...

Read More »

Mafanikio yoyote yana sababu x (1)

Wanatoka tumbo moja lakini hawafanani. Ni methali ya Tanzania. Watoto wenye wazazi walewale, walionyonya titi lile, na kusoma shule ile ile kimafanikio wanatofautiana. Kinachowatofautisha ni sababu x. Wanadarasa wakiwa na viwango tofauti vya ufaulu darasani. Inatokea aliyetangulia darasani hapati mafanikio katika maisha kuzidi aliyekuwa wa kumi. Tofauti ni sababu x. Sababu x ni siri ya mafanikio. Watu wanatoka chuo kimoja wamefundishwa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons