Monthly Archives: January 2019

TAZARA ‘imeuzwa’

Mkakati maalumu wa kuiua Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) unaohusisha kukodisha reli kwa shirika binafsi umefichuliwa, uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini. Pamoja na kukodisha reli, kiwanda cha kuchakata kokoto cha Kongolo, mali ya mamlaka hiyo kinatafutiwa ‘mnunuzi’. Uchunguzi wa miezi mitatu wa Gazeti la JAMHURI umebaini kuwa njia ya reli ya TAZARA imekodishwa kwa Kampuni ya Calabash ...

Read More »

Mfugaji ‘atapeliwa’ mamilioni

Mkuu wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Luis Bura, kwa kushirikiana na Ofisa Mifugo na Mtendaji wa Kata ya Kifula wilayani humo wanatuhumiwa kumtapeli mfugaji wilayani humo kiasi cha Sh milioni 12. Mfugaji anayedai kutapeliwa anaitwa, Subi Gagi (56), ambaye ni mfugaji na mkazi wa Kijiji cha Ilunde, wilayani Kibondo, mkoani Kigoma. Gagi ameliambia Gazeti la JAMHURI kwamba Machi 5, ...

Read More »

Chuo kutatua matatizo ya Bandari

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe amesema mafunzo yanayotolewa sasa na Chuo cha Bandari yalenge kutatua matatizo yaliyomo katika sekta ya huduma za meli, biashara za bandari na shughuli za bandari. Mhandisi Kamwele ametoa kauli hiyo katika mahafali ya 17 ya Chuo cha Bandari yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Pia Waziri alielekeza wahitimu wote ...

Read More »

Mke wa Zakaria arejea uraiani

Mke wa mfanyabiashara Peter Zakaria, Anthonia Zakaria, amekiri kosa la uhujumu uchumi na kuhukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 54. Alikuwa akishtakiwa kwa kosa hilo baada ya kujipatia mali za Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza cha mkoani Mwanza. Mali hizo ni jengo lenye ghorofa tatu na eneo kilipojengwa kituo cha mafuta, Barabara ya Nyerere jijini Mwanza. Mali hizo zilimilikiwa na ...

Read More »

Tusikubali TAZARA ifilisiwe

Habari iliyopewa uzito wa juu kwenye gazeti hili toleo la leo inahusu ‘kuuzwa’ kwa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). Mengi yamebainishwa kwenye habari hiyo, lakini lililo kubwa ni mpango wa ‘ubinafsishaji’ wake kwa kampuni ya Afrika Kusini. Tunatambua kuwa Reli ya TAZARA au kwa jina jingine Reli ya Uhuru, imekuwa ikipitia vipindi vigumu vya uendeshwaji wake. Mara ...

Read More »

Nina ndoto (4)

Muda pekee wa kutazama nyuma ni kutazama ni hatua kiasi gani umepiga. Ingawa Waswahili waliwahi kusema: “Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.” Si kila muda ni wa kusahau yaliyopita. Nyakati zilizopita zina mafunzo tunayoweza kukutana nayo kwenye wakati ujao. Kosa si kosa kama halijarudiwa. Ukirudia kosa maana yake haukujifunza muda ule ulipoanguka. Yakobo baba yake Yusufu alisahau alipotoka. Siku moja kaka ...

Read More »

Kuumbwa kwa Bonde Kuu la Ufa

Kati ya miaka 300,000 hadi 250,000 iliyopita zana kubwa za mawe zijulikanazo kama acheulian zilianza kupotea katika maeneo ya akiolojia ya Afrika. Nafasi yake ikichukuliwa na aina mpya ndogo ndogo na saizi ya kati. Ukamilisho wa zoezi hili unamaanisha mwanzo wa muhula mpya wa kifunsi uliosambaa bara zima uitwao Muhula wa Kati wa Zana za Mawe (M.S.A). M.S.A ilirudisha shauku ya kubangua ...

Read More »

Bwawa laua mamia Brazil

Watu 300 wanahofiwa kufariki dunia baada ya bwawa la maji kuvunja kingo zake katika mgodi wa kampuni ya chuma kusini mashariki mwa Brazil. Maji yaliyochanganyika na matope yaliwafunika mamia ya wafanyakazi wa shirika hilo. Shughuli ya kuwatafuta walionusurika inaendelea karibu na mji wa Brumadinho, katika Jimbo la Minas Gerais. Gavana wa jimbo hilo, Romeu Zema, amesema kuna hofu huenda watu ...

Read More »

Mzozo wa kisiasa Venezuela wasambaa kimataifa

Baada ya maandamano ya kumshinikiza Rais Nicolas Maduro kung’atuka madarakani kukumbwa na vurugu, kiongozi mashuhuri wa upinzani, Juan Guaido, amejitangaza kuwa rais wa mpito. Guaido amepata uungwaji mkono kutoka mataifa ya Marekani, Canada na majirani wa taifa hilo walio na ushawishi mkubwa katika Kanda ya Amerika Kusini kama vile Brazil, Colombia na Argentina. Muungano wa Ulaya umetoa wito wa kufanywa ...

Read More »

Rais Magufuli, Dk. Mpango jengeni wafanyabiashara (4)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala yangu kwa kushauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanzisha Kitengo cha Kuanzisha na Kukuza Biashara. Nimepata mrejesho mkubwa. Nimekuta kumbe vijana wengi wanataka kuanzisha biashara lakini hawafahamu ni wapi pa kuanzia. Sitanii, nimepata fursa ya kusoma kitabu cha Mfanyabiashara Reginald Mengi cha ‘I Can, I Must, I Will’. Ni vema nichukue fursa hii kumpongeza mzee Mengi ...

Read More »

Baadhi ya vipimo muhimu ambavyo wengi huvisahau

Vipimo ni muhimu sana kwa maendeleo ya afya zetu, kwa watu wa jinsia zote na rika zote. Kupitia vipimo tunaweza kutambua mustakabali wa afya zetu, hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri katika kupambana na maradhi mbalimbali. Hivi karibuni takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zilionyesha kuwa idadi ya wanaume watu wazima wanaopatiwa vipimo vya afya ni ndogo kuliko idadi ya ...

Read More »

Mikumi kuongeza shughuli za kitalii

Kutokana na sekta ya utalii kutiliwa mkazo na Serikali ya Awamu ya Tano kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi, Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo Kilosa, mkoani Morogoro imejipanga kuongeza shughuli za kitalii kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi. Hifadhi hiyo ina ukubwa wa kilometa za mraba 3,230, inasifika kwa kuwa na wanyama wa kila aina wakiwemo tembo, ...

Read More »

Tunafanya dhambi kuua hifadhi

Tanzania imetenga maeneo kwa ajili ya kuhifadhi maliasili na urithi wa taifa kwa kuwa na maeneo yaliyohifadhiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Wizara ya Maliasili na Utalii ndiyo iliyopewa mamlaka ya kusimamia maeneo yote yaliyohifadhiwa nchini yakiwa na sifa na hadhi tofauti tofauti. Kuna mapori ya akiba, misitu ya hifadhi, mapori tengefu, ...

Read More »

Ndugu Rais busara ni kupatana, tuwezeshee maridhiano

Ndugu Rais, kama Mwenyezi Mungu alinijalia sauti inayosikika na wengi walio karibu na walio mbali ili niwasemee waja wake, basi namwomba Muumba wetu huyo huyo awajalie baraka viongozi wetu ili wasizifanye ngumu shingo zao, bali wabarikiwe na wautegee sikio ukulele huu niupigao kama mtu aliaye kutoka jangwani:  Watoweni katika hofu watu wa Mungu ili wapate kuishi kwa amani, furaha na ...

Read More »

Barua ya wazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro

Ndugu Mhariri, Naleta hoja hii ambayo inatuhusu sisi wananchi wa Wilaya ya Kilosa kupitia Umoja wa Wakulima wa Umwagiliaji Mvumi (UWAUMVU) kuhusu uharibifu wa Skimu ya Mvumi. Skimu ya Mvumi iko katika Kijiji cha Mvumi, Kata ya Magole, Wilaya ya Kilosa, ilianzishwa mwaka 2002 na ina wanachama 298 huku eneo hilo likiwa na ukubwa wa ekari 720 zilizomo ndani ya ...

Read More »

Upuuzi na manufaa kwenye mtandao

Sina hakika kama lipo suala linaloweza kumpotezea binadamu muda wake bila manufaa yoyote kama kupitia taarifa zinazotufikia kwa njia ya mtandao. Watumiaji wa mtandao duniani wanakadiriwa kufikia bilioni 3.2 na wengi wao, kila siku wanasambaza taarifa za kila aina mtandaoni. Nyingi ya hizo hazina manufaa yoyote kwa mpokea taarifa. Wanaofaidika zaidi kiuchumi ni wamiliki wa kampuni zinazodhibiti na kuuza taarifa ...

Read More »

Trafiki akiomba leseni mwambie hivi…

Ukisimamishwa na trafiki barabarani na ukawa hauna leseni mfukoni kwa muda huo si kosa. Mwambie huyo trafiki kuwa hilo si kosa. Sheria inataka kutembea na leseni tunapoendesha vyombo vya moto, lakini pia haisemi kuwa utakapokuwa hauna pale unapoombwa na trafiki ni kosa. Tunazungumzia Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168. Wapo watu wameandikiwa faini kisa wameombwa leseni wakasema hawana, au wakasema ...

Read More »

Historia ya Sikukuu ya Valentine’s Day

“Upendo huvumilia, Upendo hufadhili, Upendo hauhusudu, Upendo haujivuni, Upendo haukosi kuwa na adabu, Upendo hauhesabu mabaya, Upendo haufurahii udhalimu, Upendo hautakabari, Upendo hustahimili yote.’’ – (1Kor 13:113). Februari 14, dunia nzima inasherehekea Sikukuu ya Wapendanao, ijulikanayo kama ‘Valentine’s Day’. Ningependa leo tufahamu sote asili ya sikukuu hii. Mwanzilishi wa sikukuu ni padri wa Kanisa Katoliki ambaye Kanisa Katoliki linamheshimu kama ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (14)

Kushindwa ni mtihani, mambo magumu sana ya kushughulikia maishani ni kushindwa na kushinda. Ukishindwa ni mtihani, ukishinda ni mtihani. Kuendeleza ushindi ni mtihani, kushikilia namba moja ni mtihani, kushikilia namba ya mwisho ni mtihani. Hoja si kushindwa bali lile mtu analofanya baada ya kushindwa. Hakuna anayefanikiwa bila kushindwa,  hakuna ambaye hufanikiwa kwa sababu ya kushindwa. “Tunaogopa kushindwa sana, kushindwa ni ...

Read More »

Rais nakuomba utafakari upya (2)

Ndugu Rais, sehemu ya kwanza ya waraka huu niliishia kwenye maneno ya hekima ya uhifadhi yaliyotolewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Agosti 10, 1975. Kwa ufupi Mwalimu alieleza matokeo ya dhambi ya kuteketeza wanyamapori na misitu iliyotendwa na Wazungu katika mataifa yao. Mwalimu alituasa tusitende dhambi hiyo. Ndugu Rais, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ...

Read More »

Tuthubutu kuondoa umaskini

Mara kadhaa nimepata kumsikia Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, akisema nchi yetu ni tajiri wakati wananchi wake ni maskini. Nchi hii imetunukiwa maliasili nyingi na Mwenyezi Mungu lakini watu wachache wametuchezea mno katika kupora mali zetu. Kauli hii inapambwa na maelezo yasemayo: “Mali hizo zingetuwezesha kuwa matajiri kama tusingechezewa na watu fulani wakiwemo ndugu zetu. Watu hawa ndio waliotufikisha ...

Read More »

Yah: Liwepo ‘bunge’ la pili la viongozi wa dini

Sijui nianze na salamu gani katika waraka wangu huu, lakini cha msingi ni kujuliana hali kwa namna yoyote ile, kwa mujibu wa waraka wangu napenda kuwajulia hali kwa namna ya salamu zenu za itikadi ya dini na protokali izingatiwe. Wiki jana Mheshimiwa Rais alikutana na viongozi wa dini pale Ikulu, kwa namna alivyokuwa akiongea nao akili yangu iligeuka na nikaona ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons