WINGA wa Arsenal, Theo Walcott amefuzu vipimo vya afya na kukubali dau la kujiunga na Klabu ya Everton. Taarifa zinaeleza, Walcott alionekana jana mchana akiingia kwenye uwanja wa mazoezi wa Everton maarufu kama , Finch Farm na leo amefuzu vipimo.

Taarifa zinadai Walcott anajiunga na Everton kwa uhamisho wa dau la paundi zaidi ya milioni £20 huku akiwa ameifungia Arsenal mabao 108 katika michezo 397 aliyoingia dimbani tangu ajiunge nayo mwaka 2006 akitokea Southampton. Walcott anakuwa mchezaji wa pili kujiunga Everton hivi karibuni baada ya Cenk Tosun.

Arsenal wanatarajia kutumia mkwanja huo wa uhamisho wa Walcott kumnasa straika wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang huku wakisubili dili la kiungo wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan ambaye wanategema kubadilishana na Alexis Sanchez.

1136 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!