Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo Mei 08, 2024 amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Pwani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl JK Nyerere Terminal I.

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo RC Chalamila amesema Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa huo zitakimbizwa umbali wa KM 427.78, kupitia miradi ya Maendeleo 39 yenye thamani zaidi ya Bilioni 479.6

Aidha RC Chalamila amesema mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zimebeba Ujumbe unaolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu “Uhifadhi wa Mazingira na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa” vilevile Ujumbe wa kudumu wa mbio za Mwenge katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria,Dawa za Kulevya, Lishe pamoja na Rushwa.

Sanjari na hilo Mkuu wa Mkoa amesema mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 utakimbizwa katika Wilaya zote za Mkoa huo ambapo Utazindua, Kukagua na Kuweka jiwe la msingi kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Mwisho Chalamila amekabidhi Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Ilala ambapo utakimbizwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhitimishwa na mkesha ambapo kesho Mei 09, 2024 Mwenge huo utakabidhiwa Wilaya Temeke.

By Jamhuri