Na Magrethy Katengu JamuhuriMedia, Dar es Salaam

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemteua aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile kugombea nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la afya Duniani (WHO) Ukanda wa Afrika kwenda kuiwakilisha nchi Tanzania.

Amebainisha hayo Leo Mei 8/2024 Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea wa nafasi ya hiyo akitarajiwa kupeperusha bendera ya Tanzania Dkt Ndugulile ambapo uteuzi huo ni kutokana na weledi na Uchapakazi wake wakati akiwa Naibu Waziri wa Afya hivyo anakwenda katika kinyang” anyiro hiko tayari hivyo hadi kufikia sasa nchi 16 zimemuunga mkono kati ya nchi hivyo Mabalozi wa nchi Rafiki na Tanazania wameombwa kuwashawishi Mawaziri wao wa Afya kumpigia kura Dkt. Ndugulile ili aweze kushinda.

Makamba amesema kuwa lampeni hiyo itahusisha mabalozi wote wa Tanzania wanaowakilisha katika nchi mbalimbali Afrika hivuo ili zoezi liwe jepesi hawana budi wanahamasisha kampeni nchi walizopo kwa kumwelezea Dkt Ndugulile wasifu wake ili aweze kupata kura za kutosha na Tanzania ing”ae kimataifa kupitia yeye kupata nafasi hiyo.

” Nimezungumza na baadhi ya viongozi wa nchi rafiki na Tanzania na kupokea majibu mazuri yakutia moyo hivyo hadi kufikia sasa nchi zote 16 za SADC zimeaihidi kuipgia kura Tanzania huku nchi nyingine saba anilizofanya nazo mazungumzo hivi karibuni zimeonesha nia ya kuichagua Tanzania katika Nafasi hiyo” amesema Waziri Makamba.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Tanzania inafanya vizuri sana katika sekta ya afya hususani katika kukabiliana na magonjwa yanayoambukiza na yasiyoyakumbukiza, kuanzia Mijini hadi Vijijini kwani huduma zimeboreshwa ikiwemo kujenga vituo vya afya huku huduma za mama na mtoto zikisogezwa karibu na wananchi ili kuepukana na adha ya kutembea mwendo mrefu kufuata huduma.

Waziri Ummy ameongeza kwa kusema pia huduma katima vituo vya afya ikiwemo za Upasuaji mbalimbali,matibabu ya moyo na mifupa ambapo anaamini kwamba Tanzania itatoa mchango mkubwa kwa Afrika katika kutunga sera bora za afya zitakazoisaidia Afrika kupiga hatua endapo mgombea wake atashinda katika kinyang’anyiro hicho.

Nae Mgombea wa Nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la afya Duniani WHO Ukanda wa Afrika Dkt Faustine Ndugulile amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kumuamini kwa kuridhia kuteuliwa kwake kuiwakilisha nchika katika nafasi hiyo huku ameahidi kuwa atahakikisha atakapopewa nafasi hivyo atakakikisha teknolojia katika sekta ya afya katika utoaji huduma Ukanda wa Afrika unaboreshwa pia huduma ya afya kwa wote kupitia bima ya afya ,kupunguza vifo vya mama na mtoto,kuimarisha mifumo ya afya kwa ujumla swala ili kuhakikisha nchi zote za Afrika zitaweza kuhimili magonjwa ya mlipuko.


” Kipamumbele changu kikuu nitahakikisha Matumizi ya tenolojia katima utoaji huduma nitafuatilia kwa kushirikiana na nchi hizi zinaboreshwa kwa kiwango cha juu kwani Dunia ipo kiganjani inawezekana Mgonjwa akatibiwa popote alipo kupitia teknolojia ” amesema Dkt Ndugulile.

Aidha latika kinyang’anyiro hicho kuna nchi 5 zimejitokeza kugombea huku nchi 47 ndizo zinazotarajia kupiga kura na upigaji kura ili apatikane mwakilishi mmoja utafanyika nchini Congo Agosti.

By Jamhuri