Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha @ACTwazalendo, Othmasoud Masoud leo Mei 08, 2024, amekamilisha ziara yake katika Mkoa wa Kigoma, ambayo imejumuisha Harakati za Kisiasa na Kijamii ikiwemo Ujenzi wa Chama.

Akiagana na Wanachama na Wananchi wa Mkoa huo kuelekea Mkoa wa Tabora, Othman alipata fursa ya kusikiliza kero za Wananchi wa Kata ya Nguruka, huko katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nguruka, Jimbo la Kigoma Kusini, ambapo pia alichangia kiasi cha shilingi laki tano kwaajili ya mwendelezo wa ujenzi wa mashimo ya vyoo vya Shule ya Sekondari Nguruka.

Awali kabla ya mkutano huo Ndugu Othman amepata fursa ya Kuzindua tawi la Chama cha ACT Wazalendo Bweru, pamoja na kupandisha bendera katika Ofisi ya chama jimbo la Kigoma Kusini.

Viongozi mbalimbali wameambatana na Mheshimiwa Othman katika Ziara hiyo, ambao ni pamoja na Kiongozi wa Chama Mstaafu ambaye pia ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kigoma Mjini, Ndugu @zittokabwe; Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Kigoma, kizamayeye na Katibu wa Mambo ya nje ya ChamaMwanaishamndeme na Waziri Kivuli wa Sera, Bunge, Ajira na Vijana, Ndolezi_Petro

By Jamhuri