Makala

Kupata hedhi isiyokoma inaashiria tatizo

Ni kawaida kwa mwanamke aliyepevuka kupata hedhi ya kila mwezi katika mzunguko wake kutokana na mabadiliko ya homoni, ambapo mfuko wa uzazi unatengeneza ukuta mpya kwa ajili ya mapokezi ya utungishwaji wa mimba. Kwa kipindi hicho mwanamke anapitia siku kadhaa za utokwaji wa damu kupitia uke. Idadi ya siku hizi imetofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine, kulingana na mfumo ...

Read More »

Sao Hill: Mgodi wa miti

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuandika makala hii kuhusu Kiwanda cha Sao Hill cha kuchakata magogo ili kupata mbao na bidhaa nyingine zitokanazo na miti au rasilimali misitu. Kiwanda cha misitu – Sao Hill Industries Ltd – ni miongoni mwa viwanda vya mazao ya misitu vilivyokuwa vinamilikiwa na serikali kupitia Shirika la Viwanda vya Misitu lililokuwa likijulikana kama ‘Tanzania Wood ...

Read More »

Rais Magufuli: Tunawapenda, tuwahitaji wawekezaji na wafanyabiashara

Hotuba ya Rais John Magufuli kwenye hafla aliyoindaa kwa ajili ya mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa kukaribisha mwaka mpya 2019 Ikulu, Dar es salaam; Machi 8, 2019   Mheshimiwa Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki;   Mheshimiwa Ahamada Fakih, Balozi wa Muungano wa Visiwa Vya Comoro na Kiongozi wa Mabalozi nchini; ...

Read More »

Mikasa ya maisha ya Kingunge

Kwa mara ya kwanza, Kavazi la Mwalimu Nyerere limechapisha kitabu kuhusu maisha ya mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale – Mwiru. Kitabu hicho kimezinduliwa Machi 6, wiki iliyopita, kikiitwa ‘Kutoka Kavazini – Mazungumzo na Kingunge wa Itikadi ya Ujamaa. Kingunge Ngombale – Mwiru 1930 – 2018.’ Kitabu hicho kimetokana na mazungumzo kati ya Kingunge enzi za uhai wake na Profesa Issa ...

Read More »

Ndugu Rais umesema wanao tumekusikia

Ndugu Rais, ukifanya vema lazima tukuambie umefanya vema. Ukiwaapisha makamishna wa Polisi, Ikulu jijini Dar es Salaam, baba ulisikika ukisema, “…Lakini kuna mambo mengine tu ambayo ni ya kawaida ambayo Jeshi letu la Polisi mnatakiwa myaelewe kwamba Watanzania siyo wajinga sana. Wanafahamu na wanajua ‘kuanalaizi’ mambo.’’ Kwa kulitambua hili baba, Mwenyezi Mungu akutangulie katika kutuongoza. Ukaendelea, “Niwatolee mfano tu alipotekwa ...

Read More »

Jumuiya ya Afrika Mashariki inayumba

Hali ya kutoelewana iliyopo kati ya Rwanda na Uganda, nchi mbili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, inatishia utangamano wa jumuiya hiyo. Uhasama kati ya nchi hizi mbili ni wa muda mrefu na umewahi kusababisha mapambano ya silaha kati ya majeshi yao ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Zipo tuhuma kutoka kila upande kwamba kuna njama za kushawishi ...

Read More »

Huwezi kubadili hatimiliki kama una mkataba serikali za mitaa

Hapo awali niliandika  namna  sheria isivyowaruhusu viongozi  wa  serikali  za mitaa  (watendaji kata, wenyeviti wa mitaa, wajumbe, na ule uongozi wote wa huko chini) kuandaa  na  kusimamia  mauzo  na manunuzi  ya nyumba au viwanja, kwa ujumla ardhi. Nikasema kuwa kitu hicho  hakiruhusiwi  katika  sheria  na wanaofanya  hivyo wako  katika  makosa  makubwa. Asilimia kumi wanayowatoza ni makosa na ndiyo maana hailipwi ...

Read More »

Tuyapende mazingira

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anasema: “Dunia ni makazi yetu ya pamoja.” Mwalimu na gwiji wa theolojia wa Kanisa Katoliki, Yohane Krisostom, naye anasema: “Dunia imeumbwa na Mungu ili kumtunza mwanadamu.” Jamii yoyote ile inayopuuza mustakabali mwema wa mazingira na uumbaji wake, ni jamii isiyojijali na isiyojali hatima ya vizazi vyake. Uharibifu wa mazingira ni aina mpya ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (20)

Kujikosoa ni mtihani, unapowanyoshea wengine kidole, vitatu vinakuelekea wewe na  kidole gumba kinasema Mungu ni shahidi. Kwa msingi huu kujikosoa ni mtihani. “Si namna tunavyofanya makosa kunakotutambulisha bali namna tunavyoyasahihisha,” alisema Rachel Wolchin. Kuna kitendawili kisemacho: “Kipo lakini hukioni.” Jibu ni ‘kisogo’. Kama kisogo kipo lakini hatukioni, kuna makosa yetu yapo lakini hatuyaoni. “Macho yangu nitazame na mimi pia.” Ni methali ya ...

Read More »

Siasa zisiwagawe mama zetu

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake yalifikia kilele wiki iliyopita. Shamrashamra zilikuwa nyingi karibu maeneo yote ndani na nje ya nchi. Wanaotambua na kuthamini utu wa mwanamke, kwao hadhi ya mwanamke iko palepale muda wote. Hawasubiri siku maalumu kulitambua au kulionyesha hilo. Mkoani Geita kuna tukio lililonishawishi kuandika haya ninayoandika leo. Si jambo zuri kwa umoja na mustakabali wa mama zetu. ...

Read More »

AINA TATU ZA SWALI Elekevu, jinga na pumbavu 

Mimi naamini mazungumzo yoyote kati ya mtu na mtu (au watu) yana maana na madhumuni yake. Yanapata uimara na thamani ya maana yanapojengewa maswali yenye nguvu ya hoja na kupata majibu yaliyosheheni ukweli na usahihi. Mazungumzo, maswali na majibu hayana budi kulandana kukidhi hoja husika kati ya mtu na mtu (au watu). Mazungumzo yasipopatiwa ustahamilivu na ukweli hayawezi kutimiza lengo na ...

Read More »

Yah: Kwanini viongozi wengi hawakufanana na Ruge?

Naandika waraka huu nikiwa najua fika kwamba kuna majonzi juu ya majonzi kwa watu wengi, hasa tasnia ya habari hapa nchi. Wengi wamesikia misiba na ambao hawajasikia ni vema wakajua sasa hata kwa kuuliza. Naandika waraka huu nikiwa na maswali mengi sana kichwani mwangu, najiuliza nimuulize nani lakini simuoni, nafikiri ni vema nikajiuliza mimi mwenyewe, Ruge ni nani? Nani alikuwa ...

Read More »

NINA NDOTO (9)

Andika maono yako Kuwa na ndoto ni ishara kwamba una tumaini. Kuwa na ndoto ni ishara kwamba unafikiri  unaweza kushinda. Kuwa na ndoto kunakufanya uonekane kijana hata kama umri unakwenda. “Kama haujawa na ndoto kuhusu kitu kipya, kitu kikubwa au kitu bora, anza kuitafuta ndoto hiyo,” anasema Dave Ramsey, mjasiriamali na mtaalamu wa mambo ya uongozi. Kuwa na ndoto tu ...

Read More »

Huduma ya mwendokasi ina mushkeli, irekebishwe

Namshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia uhai na wenye afya njema. Kila siku tukiamka ni siku mpya na yenye matumaini kwa misingi kwamba zipo fursa nyingi za kutuwezesha kuyamudu maisha yetu ya kila siku hasa katika Jiji la Dar es Salaam. Wengi wetu tunajitahidi kuchakalika hapa na pale ili kuweza kuyamudu maisha. Ili kuweza kupata riziki zetu lazima tujiharakatishe. Hapa nimetumia neno “kujiharakatisha” ...

Read More »

Ruge Mutahaba umeondoka, umetuachia funzo

Ni wiki moja sasa tangu familia, Clouds Media Group na taifa wampoteze kijana mashuhuri, Ruge Mutahaba. Baada ya wiki moja sasa tangu kifo chake, nashindwa niandike nini? Lakini sikosi cha kuandika, maana maisha ya Ruge yalikuwa kama Msahafu ama Biblia, ambako kila anayesoma anaambulia chochote. Kwanza nianze na umati mkubwa uliojitokeza katika barabara zote ambazo msafara uliobeba jeneza lake ulipita. ...

Read More »

Uhaba nyumba za walimu ni janga

Ni ukweli usiopingika kuwa pamoja na jitihada za serikali katika kuhakikisha inapunguza tatizo la upungufu wa nyumba za walimu, bado kuna changamoto kubwa kwenye sekta hii nyeti (moyo wa taifa) kwa mustakabali wa taifa! Kwa mujibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), mwaka 2010 zilihitajika nyumba za walimu 165,210 lakini nyumba zilizokuwapo wakati huo ni 46,670, hivyo kuwapo kwa upungufu ...

Read More »

Kila zama na kitabu chake, tunaona ya Awamu ya Tano

Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, kati ya mambo anayohusishwa nayo ni msemo maarufu kwamba: “…kila zama na kitabu chake.” Bila shaka msemo huu kutoka kwa mzee Mwinyi unalenga kutufanya tuwe makini ili tusichanganye mambo yanayofanyika kwa sasa na yaliyofanyika wakati mwingine hapa nchini, ni msemo unaotufanya tuondoe shaka na hali ya kujiuliza ni kwa nini hili linafanyika wakati huu na ...

Read More »

Ndugu Rais tuonyeshwe wanao busara ni kitu gani!

Ndugu Rais, Mwenyezi Mungu alipomuumba Julius Kambarage Nyerere katika nchi hii hakumuumba peke yake. Aliwaumba wengi wenye busara kama za Nyerere. Ni kipi baba kinawafanya watu wako wasione kama huwatumii wanawema hawa wengi uliopewa na Muumba wako? Hii ni kasoro ambayo wengine tunaona tuna wajibu wa kukwambia baba yetu kwa uwazi. Baba, kule ulikozaliwa ulizaliwa kama watoto wengine walivyozaliwa. Ulishuhudia ...

Read More »

Vijana ni ‘bomu’ linalohitaji kuteguliwa

Nimewahi kuandika makala kwenye safu hii nikifafanua baadhi ya faida ya taifa lolote kuwa na vijana wengi zaidi ya wazee. Bara la Afrika lina wakazi wenye wastani mdogo zaidi wa umri kuliko mabara mengine yote; Niger ikiwa nchi inayoongoza Afrika na dunia. Taarifa ya mwaka 2017 inaonyesha kuwa nusu ya raia wa nchi hiyo walikuwa na umri wa chini ya ...

Read More »

Ni kosa kisheria kudhihaki maiti

Nimeulizwa na watu wengi ikiwa agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, kuhusu kumtia mbaroni mara moja Dudubaya kwa maneno yake dhidi ya marehemu Ruge Mutahaba ikiwa ni sawa kisheria au si sawa. Ninaweka majibu wazi hapa ili hatimaye tufaidike wote, ambao waliuliza, kadhalika ambao hawakuuliza. Swali la msingi lilikuwa ni je, kuna kosa la ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (19)

Kujipenda ni mtihani si ubinafsi, kujipenda si uchoyo, wala si kujipendelea, maana huwezi kumpenda mtu kama hujipendi. Kujipenda ni kujikubali, kujithamini na kujitambua. Ushahidi kuwa watu wengi hawajipendi umejaa kama hewa, mtu anaweka vikombe vizuri vya chai kwa ajili ya wageni, yeye kila mara anatumia vikombe vilivyopasuka na vyenye mwanya, jambo hilo ni ushahidi wa kutojipenda. Fundi seremala hana kiti ...

Read More »

Demokrasia Tanzania imetundikwa msalabani (3)

Wiki iliyopita makala hii iliishia pale ilipokuwa inasema baadhi ya waandishi wameamua kuisifia serikali tu. Hapana, hii si Tanzania tunayotakiwa kuijenga. Nchi ya waoga wa kuthubutu, nchi ya wanafiki, nchi ya kujipendekeza kwa watawala. Mungu alipompa malaika Lucifer cheo cha uwaziri mkuu mbinguni, Lucifer alijisahau. Alidhani kwamba Mungu hatamtoa tena kutoka kwenye nafasi yake ya uwaziri mkuu. Jambo la kukumbuka ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons