Mwanajeshi wa Jeshi la Uganda amempiga risasi na kumuua waziri katika Serikali ya Uganda ambaye alikuwa akimlinda.

Kanali mstaafu Charles Okello Engola, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kazi, alipigwa risasi nyumbani kwake katika mji mkuu, Kampala, Jumanne asubuhi.

Haijajulikana wazi iwapo kulikuwa na mabishano kati yake na mkuu wake, kabla ya kumpiga risasi.

Baadhi ya mashahidi walisema askari huyo alizunguka kwenye maeneo jirani akifyatua risasi hewani.

Hatimaye mwanajeshi huyo, ambaye hajatambuliwa rasmi, alijipiga risasi na kufa dakika chache baadaye.

Taarifa zinasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika tukio hilo.

Video kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha wenyeji wa eneo hilo wakikusanyika katika eneo la tukio kwa mshituko.

Kanali Engola awali alihudumu kama Naibu Waziri wa Ulinzi.

By Jamhuri