Monthly Archives: March 2018

Mtibwa Sugar Wawapania Azam, Kombe la FA

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amejipambanua na amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha leo lazima wawafunge Azam FC na kutinga hatua ya Nusu Fainali Kombe la FA. Mtibwa Sugar inacheza mechi ya robo fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam na Katwila anaamini wamejiandaa hasa. “Azam wana timu nzuri lakini kweli tumejiandaa sana ...

Read More »

Pigo kwa CHADEMA, Kampeni Meneja wa Godbless Lema Ajiunga na CCM

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha kimepata pigo lingine baada ya Katibu Mwenezi wa CHADEMA ambaye pia alikuwa Meneja Kampeni wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Gabrieli Kivuyo (kushoto) amekihama chama hicho na kujiunga na CCM. Gabrieli Kivuyo amesema, amefikia uamuzi huo kutokana na utovu wa nidhamu uliopo ndani ya CHADEMA. Hii ni muendelezo wa Wanachama na ...

Read More »

Yanga VS Singida United, Kesho Mtoto Hatumwi Dukani Kombe la FA

Kikosi cha Yanga kesho kitashuka dimbani Uwanja wa Namfua kwa ajili ya kucheza dhidi ya Singida United kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la FA. Yanga ambayo ilikuwa imeweka kambi ya muda mfupi mjini Morogoro, tayari ipo Singida huku ikielezwa wachezaji wake wote wapo fiti kiafya. Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema wachezaji ...

Read More »

Tanzania Yaombwa Kuwa Mwenyeji Kombe la Kagame

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepokea barua kutoka CECAFA ikiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Kagame kwa ngazi ya klabu. TFF imepokea barua hiyo leo ikiitaka Tanzania iwe mwenyeji wa michuano hiyo ambayo mara nyingi hufanyika jijini Dar es Salaam inapotokea Tanzania kwa mwenyeji. Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amethibitisha shirikisho hilo ...

Read More »

UJUMBE WA PASAKA KUTOKA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA (KKKT)

TAIFA LETU, AMANI YETU A. UTANGULIZI “Fumbua Kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao; Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; uwapatie maskini na wahitaji haki yao” (Mithali 31: 8-9). Wapendwa wana KKKT, Watukuka, watu wote na familia ya Mungu katika Taifa letu, “Amani iwe kwenu!; Kristo Amefufuka (Yohana 20:19). Bwana wetu Yesu Kristo mfufuka, ...

Read More »

Mabula ashangaa mabilioni ‘kulala nje’

Na Munir Shemweta “Sekta ya ardhi ni nyeti kuliko sekta yoyote na iwapo itasimamiwa vizuri basi itaiingizia Serikali mapato makubwa kuliko sekta nyingine’’. Hiyo ni kauli ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, wakati akikagua Mfumo wa Ukusanyaji Kodi ya Ardhi kwa njia ya kielektroniki (GEPG) katika mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga. Katika ...

Read More »

Tuzungumze maendeleo ya watu

NA MICHAEL SARUNGI Nchi yetu ilipopata uhuru kutoka kwa wakoloni mwaka 1961 wananchi walipata madaraka ya kisiasa, hata hivyo sehemu kubwa ya uchumi bado ilibaki mikononi mwa wageni na baadhi ya Watanzania. Hali hiyo ilileta kero na ikawa mojawapo ya sababu muhimu zilizochangia kutangazwa kwa Azimio la Arusha tarehe 5/2/1967. Azimio hilo lilikuja na mkakati muhimu wa kuhakikisha wananchi kwa ...

Read More »

Yah: Kumbukizi ziakisi ukweli wa marehemu.

Kama kuna wakati nimepokea arafa nyingi za wasomaji wa barua yangu basi ni wiki jana, kila mmoja na mawazo yake, wapo waliodiriki kusema ninaegemea upande fulani kwa maslahi binafsi na wapo walionielewa na kupongeza juu ya waraka wangu ule wa wiki jana juu ya maandamano, nirekebishe; jambo muhimu lililobeba lawama zote ni kwamba mimi sikupinga maandamano bali nilizungumzia dhima na ...

Read More »

Ukataji miti hovyo unavyoathiri vyanzo vya maji Mtwara

Mashaka Mgeta, Mtwara Zaidi ya nusu ya eneo la misitu 12 inayosimamiwa na Serikali Kuu kupitia Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) mkoani Mtwara, ipo kwenye vyanzo vya maji, ikiathiriwa na ukataji miti hovyo unaovifanya (vyanzo hivyo) kuwa katika hatari ya kutoweka. Idadi hiyo ni sehemu ya misitu 51 inayosimamiwa na TFS katika Kanda ya Kusini yenye mikoa ya Lindi, ...

Read More »

Trafiki Rorya, Tarime wametuonea

Jumanne, Machi 20, 2018 ni siku ambayo hatuwezi kuisahau sisi waongoza watalii watatu. Tulifanyiwa kitendo cha uonevu wa hali ya juu pamoja na kunyanyaswa wageni watalii, raia wa Marekani tuliokuwa tukiwapeleka Sirari. Tukio hili tulifanyiwa na polisi trafiki katika wilaya za Rorya na Tarime mkoani Mara. Tulibambikiwa makosa, tukalipishwa faini na kuwachelewesha wageni, hali iliyowafanya wakasirike sana. Tulikuwa na msafara ...

Read More »

Mikutano hii iwe ya mara kwa mara

Wiki iliyopita, Rais John Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa sekta mbalimbali nchini. Masuala mengi yalizungumzwa na wafanyabiashara wenyewe, tofauti na ilivyozoeleka ambako kazi hiyo ilifanywa kwa uwakilishi. Waliopata nafasi walizungumza matatizo yanayowakabili na wakatoa mapendekezo ya kutatua kero mbalimbali. Tunampongeza Rais Magufuli na Serikali kwa jumla, kwa kuwa wasikivu. Hata hivyo, mkutano huo unaweza usiwe na tija ...

Read More »

Makazi holela kupimwa, kurasimishwa

DODOMA Editha Majura Rais Dkt. John Magufuli ameagiza wanaoishi maeneo ambayo hayajapimwa, washirikiane chini ya uongozi wa mitaa yao kupanga, kutafuta kampuni za kuwapimia makazi hayo ili kila mmoja apewe hati ya kumiliki ardhi yake. Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Dkt. Magufuli ameridhia hatua hiyo ambayo imefikiwa baada ya kubaini uwepo wa ...

Read More »

UKIPOTEZA MUDA, MUDA UTAKUPOTEZA ZAIDI

“Ukitaka kujua umuhimu wa mwaka mmoja muulize mwanafunzi ambaye amerudia darasa. Ukitaka kujua umuhimu wa mwezi mmoja muulize mwanamke ambaye amejifungua mtoto kabla ya mwezi mmoja. Ukitaka kujua umuhimu wa juma moja muulize mhariri wa gazeti linalotoka kila wiki. Ukitaka kujua umuhimu wa siku moja muulize mtu mwenye kibarua cha kulipwa kwa siku wakati ana watoto kumi wa kulisha. Ukitaka ...

Read More »

Trump apongeza mazungumzo kati ya rais Xi na Kim

Rais wa Marekani Donald Trump amesema leo kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un yuko tayari kukutana naye. Kauli hiyo inaashiria kuwa mkutano wa kihistoria unaopangwa kati yake na kiongozi huyo anayetengwa wa nchi ya bara Asia utaendelea. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Trump ameandika kuwa alipokea ujumbe jana usiku kutoka kwa rais wa China Xi Jinping ukimweleza ...

Read More »

Madereva wa Daladala Mwanza Wagoma Kutoa Huduma ya Usafiri

Mwanza Madereva wa Daladala wanaofanya safari zao Airpot Nyashishi na Kisesa Nyashishi wilayani Misungwi wamelazimika kugoma baada ya Sumatra kuongeza ruti bila kuongeza nauli. Madereva hao wamelalamikia kitendo hicho kwakuwa ruti iliyopangwa sumatra haijatoa bei elekezi nauli itakuwa sh Ngapi, kutokana na umbali. Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza Anthon Bahebe ameliomba Jeshi la Polisi kitengo cha ...

Read More »

Miguna Atimuliwa Kenya, Apelekwa Dubai kwa Lazima

Mwanasiasa wa upinzani Kenya aliyeidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa ‘Rais wa Wananchi’ Januari Miguna Miguna ametimuliwa tena kutoka nchini humo. Mwanasiasa huyo ametimuliwa huku mzozo kuhusu uraia wake ukiendelea. Bw Miguna ameandika kwenye Facebook kwamba ameamka na kujipata yuko Dubai na kwamba anahitaji matibabu. Amesema anafahamu kwamba kuna mpango wa kumpeleka London lakini anataka kupanda ndege ...

Read More »

AGPAHI YAKABIDHI MASHINE ZA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI,KOMPYUTA MKOA WA MWANZA

Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi mashine tano za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’ mkoa wa Mwanza.    Msaada huo umetolewa Jumanne Machi 27,2018 katika ukumbi wa mikutano wa Gold Crest Hotel jijini Mwanza wakati wa kikao cha wadau wanaohusika katika mapambano ya VVU na Ukimwi mkoani Mwanza kwa ajili ya ...

Read More »

Kichaa cha mbwa chatesa K’njaro

Mamlaka za Serikali zimetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa wilayani Moshi na maeneo mengine mkoani Kilimanjaro. Februari, mwaka huu, watu watatu walifariki dunia wilayani Moshi, chanzo kikielezwa kuwa ni kung’atwa na mbwa wenye kichaa. Watu 64 wameripotiwa kujeruhiwa na mbwa wenye ugonjwa huo katika vijiji vya TPC, Mawala, Oria, Mabogini na Ngasini. Waliofariki ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons