Habari za Kitaifa

Rais Magufuli Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere

Rais Dkt. Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwl. Julius Nyerere kilichopo Kibaha, Pwani. Chuo hicho kinajengwa kwa gharama ya Sh. Bil 100, kwa ufadhili kutoka chama cha CPC cha China kwa ajili ya vyama 6 vya ukombozi Africa (CCM, ANC, ZANU-PF, Frelimo, MPLA na SWAPO na kitachukuwa miaka miwili mpaka kukamilika kwa ujenzi. ...

Read More »

Lugola Ampa Siku 10 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya vitambulisho- NIDA

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola ametoa siku zisizozidi kumi kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya vitambulisho NIDA, akiwa na kampuni ya Iris Dilham kufika ofisini kwake mjini Dodoma ili kueleza sababu ya kutofika kwa mtambo wa kuchapisha vitambulisho mpaka sasa. Agizo la Mh. Lugola linakuwa ni utekelezaji wa miongozo aliyopatiwa na Rais Magufuli siku alipomuapisha kuwa Waziri ...

Read More »

Mgombea wa Udiwani Kata ya Turwa, Tarime Kupitia CCM Amepita Bila Kupingwa

Mkurugenzi wa Halamshauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa ameamua kumutangaza aliyekuwa Mgombea udiwani kata ya Turwa kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Bw Chacha Mwita Ghati kwa madai kuwa amepita bila kupingwa huku akieleza kuwa wagombea Wenzake kutoka vyama vya upinzani wamekosea kujaza fomu jambo ambalo lilisababisha msimamizi Msaidizi wa wa uchaguzi ambaye ni Afisa Mtendaji wa kata kutowateua ...

Read More »

WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU MICHANGO YA SHULE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hakuna michango yoyote itakayokusanywa kutoka kwa wazazi kwa ajili ya shule kama haina kibali cha Mkurugenzi wa Halmashuri.   “Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli alishapiga marufuku michango ya aina hii na akatangaza mpango wa elimumsingi bila malipo. Sasa hivi zinaletwa zaidi ya sh. bilioni 20 kila mwezi kwa ajii ya kuboresha elimu ya ...

Read More »

WAZIRI MKUU AWAONYA VIONGOZI WAPYA WA SHIRECU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wapya wa Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga wajipime kama wako tayari kuwatumikia wananchi na kama sivyo waachie ngazi.   Ametoa onyo hilo jana (Ijumaa, Julai 13, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa kijiji cha Mwangongo na vijiji vya jirani mara baada ya kukagua soko la pamba kwenye kijiji hicho, wilayani Kishapu mkoani ...

Read More »

RAIS DK. MAGUFULI ATENGUA NA KUTEUA MKURUGENZI MKUU NSSF

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara kuanzia leo 14 July 14, 2018. Prof. Kahyarara atapangiwa kazi nyingine. Kufuatia hatua hiyo, Rais Magufuli amemteua William Erio kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF. Kabla ya uteuzi huo Erio alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa ...

Read More »

HABARI PICHA: Mke wa Kibonde azikwa Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam

  Jana  July 13, 2018 Familia, ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na mtangazaji Ephraim Kibonde wameuaga na kuuzika mwili wa marehemu Sara Kibonde ambaye ni mke wa mtangazaji Kibonde nyumbani kwake, Ubungo Kibangu na kisha baadae kuupumzisha mwili wake katika makaburi ya Kinondoni.

Read More »

TAZAMA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

BARAZA la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza matokeo ya kidato cha sita leo Julai 13 na kuzitaja shule zilizoshika mkia kuwa ni pamoja na ya wasichana ya Jangwani, ya Jijini Dar es Salaam. Ubora wa ufaulu kwa watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 72,866 sawa na 95.52% wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu wakiwemo wasichana 30,619 ...

Read More »

Mkanganyiko rangi za mapaa Dodoma

Uamuzi wa Baraza la Madiwani wa Jiji la Dodoma wa kutofautisha kwa rangi mapaa ya nyumba kwenye kata zote 41 umepokewa na wananchi kwa mitazamo tofauti. Uamuzi huo ulifikiwa kwenye kikao cha robo ya pili ya mwaka, Januari, mwaka huu na utekelezaji wake ulipaswa uanze Machi, mwaka huu. Baadhi ya wananchi wanalalamikia ukubwa wa gharama zinazowakabili ili kubadili rangi kulingana ...

Read More »

Tume anayoitaka Mke wa Bilionea Erasto Msuya iundwe

Upande wa Mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41), umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) analifanyia kazi. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa. Wakili Mwita amedai kuwa ...

Read More »

DAWASCO YATAKIWA KUWEKA MITA ZA KIELEKTRONIKI

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakati wa ziara ya kujitambulisha mapema leo ofisi za DAWASCO. Picha zote na Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG. Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja alitoa maelekezo ...

Read More »

KAMANDA SIRO AFANYA MABADILIKO YA MA-RPC

  Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Siro amefanya mabadiliko ya Makamanda katika baadhi ya mikoa kama ifuatavyo. 1. SACP Deusdedit Nsimeki aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi anakwenda kuwa RPC Simiyu. 2. SACP Ulrich Matei aliyekuwa RPC Morogoro, anakwenda kuwa RPC Mbeya. 3. Kaimu RPC Mkoa wa Mbeya, ACP Mussa Taibu amehamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi 4. SACP ...

Read More »

MAJIMAREFU KUAGWA KESHO DAR, NA KUZIKWA ALHAMISI YA TAREHE 5/07/2018, KOROGWE, TANGA

Aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu enzi za Uhai wake. Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu, utaagwa kesho Julai 4, 2018 na baadaye mwili kusafirishwa kuelekea jimboni kwake Korogwe kwa ajili ya maziko Julai 5,2018. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe mkoani Tanga Hillary ...

Read More »

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BAADHI YA VIONGOZI WAKUU NA VIONGOZI WASTAAFU IKULU DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiiongozi Balozi John Kijazi akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam ili kukutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wakuu na viongozi wastaafu ambao anakutana nao kwa mara ya kwanza wote kwa ...

Read More »

Gari Lateketea kwa Moto Daraja la Kigamboni

MOTO umewaka na kuteketeza gari dogo aina ya Toyota Ractics, leo Jumatatu, Julai 2, 2018 katika Daraja la Nyerere (Kigamboni) jijini Dar es Salaam huku mwenye gari akifanikiwa kutoka nje ya gari na kukimbilia sehem salama. Chanzo cha ajali hiyo imedaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme wa gari hiyo pindi limefika kwenye kukata ticket hitilafu hiyo imetoka na kuanza kuungua, ...

Read More »

Kauli ya TCRA Zanzibar Kuhusu Usajili wa Blog

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, kanda ya Zanzibar, imewatoa wasiwasi wamiliki wa tovuti, blogi, redio na televisheni za mtandaoni, kuwa usajili utashughulikiwa na Tume ya Utangazaji Zanzibar na sio TCRA. Hayo yanakuja kufuatia tangaazo la hivi karibuni la TCRA, la kuwataka wamiliki wa mitandao hayo kusajili haraka vyinginevyo hawataruhusiwa kutoa huduma. Baadhi ya mitandano, ukiwemo mtandao maarufu wa Jamii Forum, ...

Read More »

Peter Msigwa Asema Wabunge wa CCM Wanampaka Mafuta kwa Mgongo wa Chupa Rais Magufuli

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, akichangia hoja katika mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya serikali 2018 / 2019 iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango, amemvaa waziri huyo wa fedha, na kumwambia kwamba alipoanza kuhutubia alianza kwa nadharia, na hakusikiliza kuhusu kodi ambazo ametoa zingeleta matatizo kwenye uchumi hakusikiliza. Mh. Msigwa amesisitiza kuwa ...

Read More »

RC Katavi awaita wawekezaji Kiwanja cha Ndege Mpanda

MKUU wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga amewaita wawekezaji wa usafiri wa anga kuwekeza kwenye Kiwanja cha Ndege cha Mpanda, kutokana na kuwa na miundombinu mizuri. Meja Jenerali mstaafu Muhuga amesema hayo kwa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), iliyofanya ziara kwenye kiwanja hicho, ambapo ameihakikishia wapo abiria wengi wa kutosha. ...

Read More »

HALI YA MWARABU FIGHTER BAADA YA KUPATA AJALI NA KUPASUKA KICHWA

Kufuatia Bodigadi wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, Mwarabu Fighter aliyepata ajali mbaya alfajiri ya leo katika eneo la Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam na kupasuka kwenye uso, majeruhi huyo ameeleza kuwa kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa huduma ya kwanza katika Hospitali ya Lugalo iliyopo Mwenge jijini Dar kisha kuhamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Akizungumza kwa ...

Read More »

Serikali haitafuta tozo daraja la Kigamboni

Serikali imesema kuwa haitafuta tozo inayotozwa katika daraja la Kigamboni kwa kuwa fedha hizo zinatumika kulipa sehemu ya deni la mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Juni 22,2018 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu Antony Mavunde akisema kwa sasa utaratibu unaandaliwa ili wavukaji wawe na hiyari ...

Read More »

Mwenyekiti CHADEMA Ashambuliwa kwa Mapanga na Mishale

MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Mwikatsi wilayani Babati mkoani Manyara, Simon Lala (CHADEMA) ameshambuliwa na kujeruhiwa kwa mishale na mapanga na watu wasiojulikana kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi.     Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa shambulio hilo limetokea jana Juni 18, 2018 katika Kitongoji cha ...

Read More »

Tanzia: Profesa wa Upasuaji Chuo Kikuu Muhimbili Afariki Dunia

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof. Adrea Pembe anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Leonard Lema kilichotokea leo asubuhi tarehe 18 Juni 2018 katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Prof. Lema alikuwa ni Profesa katika Idara ya Upasuaji katika Skuli ya Tiba MUHAS. Wakati wa uhai wake, Prof. Lema ametumikia Chuo katika nyadhifa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons