Na Magrethy Katengu,JamuhuriMediia Dar es Salaam

WAKALA wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) leo wamefunga mafunzo kutoka kwa wataalamu wa idara ya Tehama ambayo yamejikita katika kadi janja zitakatumika katika mfumo wa nauli kabla ya abiria kuiingia kwenye geti anatumia kadi badala ya kulipa nauli keshi.

Akizungumza leo Mei 17,2024 Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dart, Athumani Kihamia wakati wa kufunga mafunzo hayo siku tano kwa wahitimu 10 yaliolenga utunzaji wa usalama za kadi janja na nywila zake kutoka kampuni ya Advan IDe kutoka nchini India.

Hata hivyo Mkurugenzi amefafanua kuwa, hadi sasa mageti zaidi ya 300 yaliyogharibu zaidi ya bilion 11 na ujenzi wake umeshaanza na kufikia asilimian67 itasidia kudhibiti mapato kwa watumishi wasio waaminifu,.

“Kadi janja ni kadi zinazotumika katika mfumo wa nauli lengo la DART ni kufunga maeneo mengi wakiwa na timu kubwa ya vijana mahiri ambao tutakaa nao kwa miaka 10 ili iwe rahisi kupeana ujuzi na vijana wengine wapya watakao ajiriwa, tunataka kuboresha mifumo yetu ili tutoe huduma zenye ubora”amesema Kihamia.

Hata hivyo, amesema kuwa siku chache zijazo baada ya mwezi wa sita wataanza kutumia mageti hayo ambapo wameshaingiza mageti janja kutoka nje zaidi ya 300, yatatumika katika mfumo wa nauli yataepusha wizi wa mapato kwa watumishi wasio waaminifu, pamoja na kuokoa muda wa kukaa muda mrefu kituoni

Naye Mkurugenzi wa teknolojia habari na mawasiliano Dart Ng’wanashigi Gagaga amesema baada ya Mafunzo ya kujenga uwezo wa timu ya wanaoshughulikia mfumo wa nauli katika mageti yatakayotumia na kadi ambapo mpaka sasa kituo cha Korogwe kimeshakamilika na vingine vinaendele na matengenezo.

“Ubora wa Mageti haya janja yatakayofungwa mfumo maalumu na kuanza kutumika abiria atakapofika na kadi yake itamwonyesha kiasi cha fedha kama hakitoshelezi akaongeze hivyo hakutakuwa na matumizi yeyote ya karatasi tuko kidigital zaidi ” amesema Mkurugenzi Tehama .

Naye Muhitimu wa Mafunzo hayo Jackson Kazaura ameshukuru kupata mafunzo hayo hivyo ameahidi ujuzi huo anakwenda kuutumia na kufundisha wengine .

Naye Mwakilishi wa Wataalamu Kampuni waliyotoa mafunzo Kadi janja Advan IDe, Duncan Chege amesema wanaamini mafunzo hayo waliyotoa wakufunzi wataenda kutekeleza progaram hiyo kwa weledi zaidi huku wakiwafundisha na wengine ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria .

Aidha onyo kali limetolewa kwa madereva wanaoendesha magari ya serikali na maboda boda na magari binafsi kuacha mara moja kutumia njia ya mwendokasi bila kibali maalum kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria na kusababisha ajali zisizo za lazima.