Jumla ya ajali 18 zimeripotiwa mwezi wa Aprili, 2024 Wilaya ya Kaskazini ‘A’ na Kaskazini ‘B’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi ambazo ni nne (4) kwa kila wilaya sawa na asilimia 22.2 ikilinganishwa na wilaya nyengine.

Akitoa taarifa ya Makosa ya Barabarani Mtakwimu kutoka Kitengo cha Makosa ya Jinai, Madai na Jinsia katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar Asha Mussa Mahfoudh amesema idadi ya ajali za barabarani zilizotokea kwa Aprili, 2024 zimeongezeka kwa asilimia 28.6 kufikia ajali 18 kwa mwezi wa Aprili 2024 kutoka ajali 14 mwezi wa Machi 2024.

Amesema kwa mwezi wa Aprili 2024, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ na Kaskazini ‘B’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi (ajali nne (4)) kwa kila Wilaya ambapo Wilaya ya Kati iliripotiwa kuwa na ajali zaidi (ajali tatu (3)) kwa mwezi wa Machi 2024.

Aidha, Idadi ya Ajali za barabarani kwa mwaka zimeongezeka kwa asilimia 28.6 na kufikia ajali 18 kwa mwezi wa Aprili 2024 kutoka ajali 15 kwa mwezi wa Aprili 2023.

Kwa mwezi wa Aprili 2024, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ na Kaskazini ‘B’ imeripotiwa kuwa na ajali nne (4) kwa kila wilaya na Aprili 2023 wilaya ya Magharibi “A” ilikuwa na ajali zaidi, nne (4).

Nao Askari Polisi ambao ndio wadau wakubwa wa ajali za barabarani wameiomba jamii kuchukua tahadhari kwa kila jambo ambalo husababisha ajali ikiwemo Bodaboda wanaofanya kazi hiyo bila ya vibali maalum pia mtindo wa Bodaboda kupakia watoto wengi kwa wakati mmoja wakati wa kuwapeleka skuli na kuwarudisha.