-Afungua na kufunga Kikao kazi Cha Robo Mwaka

-Aelezea Umuhimu wa Kikao kazi Cha Robo Mwaka

-Atoa Maagizo yafuatayo kwa MSM na Taasisi za Serikali Dsm

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.Toba Nguvila amezitaka Taasisi za Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) kushirikiana vema katika kutoa huduma kwa wananchi na sio kutunishiana misuli wao kwa wao

Dkt. Nguvila ameyasema hayo Mei 17, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglo uliopo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha robo mwaka ambacho kilifanyika kwa Mara ya mwisho 2019.

RAS Nguvila ameongeza kuwa uratibu na Usimamizi wa Kikao kazi hicho unafanywa na Sekretarieti ya Mkoa kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Tawala za Mikoa Sura namba 97 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2002

Aidhaa, Katibu Tawala ameeleza kuwa Kikao kazi hicho ni muhimu kwa ajili ya kumuwezesha kupata taarifa za utekelezaji wa Miradi, Ukusanyaji wa mapato na utendaji kazi wa jumla wa Halmashauri na Taasisi za Umma zilizopo ndani ya Mkoa

Dkt. Nguvila ameyataja maagizo mbalimbali yaliyotolewa na Mamlaka Kama vile:-
-Matumizi ya Mifumo ya kielektroniki katika Ukusanyaji wa mapato, Watendaji wa Serikali kwenda “field” kusimamia miradi sio kukaa ofisini, Watendaji kutatua kero za wananchi, Kujibu Hoja za Ukaguzi kwa wakati, Kudhibiti matumizi ya fedha za umma, Wabadhirifu wa fedha za Umma kuchukuliwa hatua stahiki, Ulipaji wa Madeni ya watumishi, Kuboresha na Kupendezesha Mandhari ya Jiji la Dsm, Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa dhidi ya Rushwa, Matumizi ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ikiwemo matumizi ya mfumo wa NEST na Utekelezaji wa Mfumo wa “Pepmis na Pipmis”.

Hata hivyo, RAS Nguvila ametoa maagizo yafuatayo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Serikali Kama ifuatavyo:-
-DAWASA– kuona namna ya kuwarejeshea huduma wadaiwa sugu waliokatiwa maji miaka mitano au zaidi kwa kuweka mikataba mipya ya ulipaji kwa lengo la kupanua wigo wa kukusanya mapato -TRA na MSM – Elimu ya EFD itolewe na iwe endelevu
-TANESCO– Wakandarasi wanaochelewesha miradi ya Maendeleo wachukuliwe hatua kwa mujibu wa mkataba ikiwemo kuvunja mkataba
-TARURA,TANROADS na MSM– Malori yote yanayopaki barabarani yaondolewe Mara moja.


-BONDE LA RUVU– taratibu za kuchimba mchanga zifuatwe, Kodi ilipwe, Vibali visitoke ovyo ovyo, mifugo ikiingia ipigwe faini kwa mujibu wa Sheria na usimamizi wa uchimbaji wa visima
-NEMC– Yatakiwa kushauri Mahali pa kupelekea maji machafu yanayotiririka kutoka viwandani
-MSM na Taasisi za Serikali kuelezea kwa wananchi miradi ya kimkakati inayotekelezwa (inayofanywa) na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Ikumbukwe kuwa Kikao kazi hicho kilikuwa Cha siku mbili yaani tarehe 16 -17 Mei, 2024 ambapo watendakazi hao walitumia kikao hicho kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi katika maeneo yao.

By Jamhuri